Habari za asubuhi mpendwa mfuatiliaji wa Mpeke blog, leo ningependa tujifunze juu ya vipindi 7 vya maisha ya kazi na uzoefu wa maisha ambavyo unatakiwa uvipitie pindi uwapo hai hapa Duniani.
1. Kabla ya miaka 20. Unatakiwa uwe mwanafunzi mzuri na unapenda kujifunza mambo mbalimbali.
2. Miaka 20 - 25. Ni kipindi cha kujalibu mambo mbalimbali na kufanya makosa mengi, na wanasema katika kipindi cha miaka 25, hiki ni kipindi ambacho unatakiwa uthubutu na kufanya makosa mengi ili uweze kujifunza kupitia hayo makosa.
3. Miaka 25 - 30. Katika kipindi hiki kijana unatakiwa uwe chini ya mtu muhimu/ maalumu utakayejifunza mambo mbalimbali kutoka kwake ( This is the period which you need to have a mentor ). Fanya kazi chini ya taasisi ndogo ili uweze kupata nafasi ya kujifunza mambo mengi kwa sababu kutakuwa na uangalizi wa karibu, utaonekana makosa yako, nguvu zako na madhaifu yako na pia utaweza kusaidiwa. Katika hili pia utajifunza kuwa na uvumilivu, kuchukuliana na watu tofauti tofauti, unyenyekevu, ukomavu, jinsi ya kuwa na maono na kutimiza ndoto zako.
Kipindi hiki siyo unafanya kazi kwenye kampuni gani ila unafanya kazi chini ya bosi gani ( Not which company you go, but which boss you follow )
4. Miaka 30 - 40. Katika hiki kipindi unatakiwa ufikilie kwa makini ni jinsi gani utakamilisha maono yako.
5. Miaka 40 - 50. Hiki ni kipindi cha kufanyia kazi kile kitu ambacho unauwezo nacho tu, Hiki ni kipindi cha kufanyia kazi kitu kile ulichonacho ambacho ni mzuri katika hicho kitu. Fanyia kazi kitu ambacho unauwezo nacho na siyo kujaribu kila kitu. Usijaribu kufanya kitu kipya katika hiki kipindi.
6. Miaka 50 - 60. Hiki ni kipindi ambacho mtu anatakiwa kuwekeza kwa vijana kwa sababu vijana wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi nzuri kuliko wewe.
7. Kuanzia miaka 60 na kuendelea. Hiki ni kipindi cha kutumia muda wako mwingi kula maisha yako vizuri binafsi. Pata muda mwingi wa kupumzika na kufurahia maisha.

Ni matumaini kuwa umepata kujifunza, nikutakie tafakari njema na siku njema.

0 comments:

Post a Comment

 
Top