Kuhailisha kufanya jambo (Procrastination)
Procrastination hii ni hali kuhairisha kufanya jambo. Hakuna ugonjwa mbaya wa mafanikio kwa binadamu kama ugonjwa wa kuhailisha kufanya vitu, kwa lugha ya kizungu unaitwa PROCRASTINATION
Hii ni hali ya kuhairisha kufanya jambo, unaweza ukawa unatamani kufanya jambo fulani ambalo litakuletea faida kubwa hapo baadaye, au unatamani uanzishe biashara na uwezo unao lakini kila unapotaka kuanza unajisemea nitaanza kesho, au nitaanza week ijayo, mwezi ujao au mwakani. Au kama wewe ni mwanafunzi kila ukitaka kusoma unasema nitasoma kesho.
Na hii pia inaweza ikawa ni sababu kwa nini watu wengi hatupigi hatua kuendelea mbele.
Kuwa makini sana kama hali hii inakutokea, badala yake anza haraka kufanya hilo jambo wala usisubilie kufanya baadaye au kesho maana wakati uliokubalika wa kufanya mabadiliko ni sasa, siyo kesho wala kesho kutwa.
0 comments:
Post a Comment