Katika maisha ya binadamu yoyote kuna vipindi huwa anapitia pindi anapozaliwa mpaka anapokufa, leo ningependa nikukumbushe hivyo vipindi 6 kwa uchache
1. Mwaka 0 - 15 Hiki ni kipindi cha kuishi kwa maono ya mzazi, katika umri huu mtoto anategemea kila kitu kutoka kwa mzazi
2. Miaka 15 - 25 Hiki ni kipindi cha kupata maono ( Dreaming season ) Hiki ni kipindi ambacho unapanga unataka kuja kuwa nani kwa hapo baadaye, ni kipindi ambacho unatakiwa uwe na vision ( You must have a vision ) na unatakiwa upange kuwa unataka uwe wapi miaka ijayo kiuchumi au katika ngazi ya familia hata kama mazingira au uchumi hauruhusu, unatakiwa ujipange
3. Miaka 25 - 35, Hiki ni kipindi cha kufanyia kazi maono yako yale uliyokuwa nayo katika kipindi cha miaka 15 - 25
4. Miaka 35 - 45, Hiki ni kipindi cha kuyaishi na kuyatumikia maono yako baada ya kutimia ( You live your vision)
5. Miaka 45 - 70, Hiki ni kipindi cha kuacha urithi na kuwawezesha wengine. Hiki ni kipindi cha kuwekeza hazina kwa watu vijana, unatakiwa uwafundishe vijana juu ya shughuli unazozifanya ili waweze kuendeleza maono yako.
6. Miaka 70 - 100, Hiki ni kipindi cha kusubilia umalize safari yako ya Duniani. Ni kipindi ambacho unasubilia geti lifunguke upeleke ripoti.

Hakikisha kila kipindi unakitumia vizuri ili usiweze kujuta hapo baadaye. Tafakari njema na jioni njema

0 comments:

Post a Comment

 
Top