Kwanza nipende kuwapongeza wote mliohitimu masomo yenu kwa huu mwaka ( Congratulation because you made it ) na pia nipende kushukuru kwa kuwa nimekuwa nikialikwa kwenye mahafali yao vyuo tofauti tofauti kutoka kwa jamaa zangu, rafiki zangu pamoja na ndugu zangu.
Leo ningependa kuwakumbusha mambo machache wasomi wote mnaohitimu kwa vyuo vyote nchini
- Kwanza ningependa mjue ni nini maana au lengo la elimu mliyoipata. Maana halisi au lengo la elimu ni kuondoa ujinga akilini mwako ili uwe na akili ya kujua kipi Unatakiwa ukifanye baada ya kutoka katika huo ujinga.Lakini chakushangaza wengi wetu tunasoma tukiwa na matumaini makubwa ili tuje tuajiriwe, tukiamini kuwa kazi nzuri ni ile ya ofisini tu na tukishindwa kuajiriwa elimu yetu inakuwa imeishia hapo. Hapa ndo tunakutana na kizazi cha wasomi wanaozunguka maofisini na bahasha za kaki miaka miwili wakitafuta kazi bila kupata, Just imagine! Hautakiwi kuwa hivyo, fikilia nje ya box kuitumia elimu yako ili uweze kujiajiri.
- Pili, ningependa niwakumbushe kuwa mtaani mnapoingia kuna wasomi wengi kama nyinyi, tukianzia na waliomaliza 2015 na 2016 ambapo wengi wao bado hawajaajiriwa na hawana kazi, na nyie mliomaliza huu mwaka 2017. Hivyo ukishindwa kuwa mbunifu na kujitofautisha na wasomi wengine, utaishia kuilaumu serikali kwamba ajira hamna. Rejea juu nini haswa lengo la elimu uliyoipata.
- Tatu na mwisho, Pia ningependa mjue kuwa shuleni tulikuwa tunafundishwa jinsi ya kujitegemea wenyewe, tukikatazwa kusaidiana kwenye chumba cha mtihani. Lakini huku mtaani ili uweze kufanikiwa unahitajika kuishi vizuri na watu pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana na wenzako ( team work ). Wote waliofanikiwa wanafanya kazi kwa ushirikiano na ukiwa mbinafsi nikukumbushe kuwa hauwezi kufanikiwa. Unapomuona Bhakhresa au Mengi au yeyote yule aliyefanikiwa jua kuwa kuna watu wanaofanya nao kazi na wanategemeana. Kwa hiyo jifunze kushirikiana na wenzako ili uweze kufanikiwa.
Ni matumaini yangu kuwa umepata mambo mawili matatu yatakayokusaidia kuingia nayo uraiani.
Imeandaliwa na Geofrey Mpeke.
Imeandaliwa na Geofrey Mpeke.
Kwa
kumalizia nikuache na wimbo huu ukisema kuwa This world is yours
usiogope kuthubutu, kama utaamini kile unachokifanya hakika kitakuwa
vile unavyoamini.
Shukrani Mr.Mpeke
ReplyDelete