1. Utambulisho ( The identity )
Wewe ni nani na unajijua kama nani au unajiona kama nani! Je ni mtu aliyeshinda au mtu aliyeshindwa. Wengi wetu tunashindwa kupiga hatua kwa kujishusha na kujiona kuwa hatuwezi kufanya vitu vikubwa. Na hii inapelekea hata wanafunzi mashuleni kuona kwamba hawawezi kuwa wa kwanza darasani eti ni kwa sababu kuna mtu huwaga anakuwa wa kwanza katika mitihani. Jikubali kwanza wewe mwenyewe maana ukijikubali wewe na wengine watalazimika kukukubali, aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.( make a good self image ) Tengeneza jina lako kwa kujiona kuwa unaweza kuwa vile utakavyo.

2. Uhusiano wako na Mungu.
Wengi wetu tunategemea akili zetu katika kufanya mambo yetu na kumsahau Mungu aliyetupa uwezo wa kufanya hivyo vitu, na hiki ndo kikwazo cha kwa nini watu hatufanikiwi katika mambo yetu. Ili uweze kufanikiwa unatakiwa uwe karibu na Mungu na uweze kufanya kazi na yeye kwa kumshirikisha.

3. Hofu na uoga
Watu wengi wanajiongelea vibaya kabla hawajaanza kufanya jambo kwa kuwa na hofu nyingi pamoja na uoga wa kuanza. Kwamba itakuaje kama nitashindwa kufanikiwa katika hili!
Visingizio, watu wengi huwa na visingizio vingi kabla hawajaanza kufanya jambo, mbona wale walifanya lakini wameshindwa. Hii yote ni kwa sababu ya uoga pamoja na hofu ya kuanza kitu kipya ambazo watu wamejiwekea na vinawasababishia washindwe kupiga hatua kuelekea kwenye mafanikio yao.

4. Kuangalia mapungufu yako. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wanaangalia mapungufu walionayo kuliko kuangalia nguvu ( strength ) walizonazo. Mwingine anajiona hawezi kufanikiwa eti kwa sababu amezaliwa katika familia masikini. Au mwingine anasema siwezi kufanya hiki kwa sababu eti sijasoma hapana jaribu  acha kuwa na visingizio visivyo na maana. Mwanasayansi mmoja Albert Einstein alishawahi kusema “kila mtu ni gwiji" hivyo basi usichukulie mapungufu yako kama kikwazo cha wewe kupiga hatua bali iwe ni nguvu ya wewe kusonga mbele.

5. Kujilinganisha.
Watu kabla hawajaanza kufanya jambo au biashara wanajilinganisha na wengine waliofanikiwa na kujidharau kuwa wao hawawezi. Usijilinganishe na watu wengine kwa sababu kila mtu ana njia yake ambayo Mungu amemkusudia ili aweze kufanikiwa, kuna msemo unasema slow but sure. Hivyo hivyo kwa kufanya kidogokidogo unaweza kufanikiwa usiwatazame watu jinsi walivyo na kasi kwenye kupata mafanikio.

Mwisho niseme kwa kumalizia, Tamani kuwa na maisha ambayo Mungu amekukusudia kufika kwa kuangalia maono yako. Usiruhusu au kukubali mtu yeyote yule akakurudisha nyuma. Focus on your vision.

0 comments:

Post a Comment

 
Top