Watafiti wamefanya utafiti na kugundua kuwa kuna aina 4 za mitindo ya malezi nayo ni;

1. MTINDO WA MALEZI YA KIMABAVU ( Authoritarian parenting )
huu ni mtindo wa malezi ambao siku zote wazazi huwa ni wakali. malezi haya huwaacha watoto wao katika majeraha tangu wakiwa wadogo mpaka wanapokuwa watu wazima. Na watoto wanaolelewa kwa mtindo huu wa malezi mara zote wanakuwa hawana upendo kwa wazazi wao wenyewe, kwao wenyewe na hata kwa watu wengine. Mtindo huu ndo unaosababisha kuwepo na majambazi na watu wasio na huruma katika jamii

Sifa za wazazi wanaowalea watoto wao kwa mtindo wa malezi ya kimabavu
  • Kuwabebesha watoto mzigo wa kanuni na sheria nyingi. Mtoto anahitaji uhuru katika ukuaji wake, hapaswi kuwa na sheria nyingi zitakazomuumiza na kusababisha kujisikia kama mtumwa
  • Kufanya mambo yanayomuabisha mtoto bila kujali hisia zake. Kama kumchapa mtoto mbele ya marafiki zake au kumuadhibu mbele ya wenzake, Kwa kufanya hivyo unasababisha kumuua utu wake wa ndani na kumfanya apoteze upendo na wewe. Usimlinganishe mtoto wako kwa kumsifia mwenzake na kumsema yeye vibaya, mtoto hatakiwi kukandamizwa ila anatakiwa kutiwa moyo.
  • Kutowahusisha watoto kwenye mambo yoyote ya kifamilia. Kwa kuwashirikisha watoto kwenye maamuzi ya kifamilia utawajengea uwezo mzuri wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi hata pindi watakavyokuja kuwa watu wazima.
  • Kutowapa watoto sababu zozote kwa kila hatua mzazi anayoichukua juu yake. Hasa hasa tineja, unatakiwa ukiwa unampa ushauri  mpe na sababu usitumie mabavu na nguvu, kwa mfano ukimuambia aache tabia unayoiona kuwa ni mbaya kwake unatakiwa umpe na sababu kwa nini anatakiwa aiache.
  • Kutumia adhabu zisizo na mafundisho wala  marekebisho kwa mtoto. Adhabu zinapaswa zibebe fundisho ndani yake, usimuadhibu mtoto wako kwa hasira kwa maana utatengeneza mtoto mkatili na mwenye kiburi. Muadhibu mtoto kwa upendo, usikimbilie kumuadhibu mtoto kabla haujampa fundisho juu ya kile alichokosea na kwa kufanya hivi utamjengea mtoto mazingira ya kukupenda.
Muhimu: Mtoto hatakiwi kukuogopa ila anatakiwa kukuheshimu, ukiona mtoto anakuogopa jua kuwa unamlea malezi ya kimabavu.

Athari zinazomkuta mtoto aliyelelewa kimabavu
  1. Tatizo la kutojiamini na kujikubali.
  2. Tatizo la kutokuwaamini wengine.
  3. Kuwa watu wakali na wanaotumia mabavu.
  4. Kuwa na hofu na wasiwasi mara kwa mara ( Anxiety ).
  5. Watoto kuwa wakorofi wanapokuwa mbali na wazazi wao.
  6. Kuwa na nidhamu ya uoga.
  7. Kuwa na kiwango kidogo cha kufanya maamuzi yanayowafaa ( Poor decision making )

2. MALEZI YA KUDEKEZA ( PERMISSIVE PARENTING )
Haya ni malezi ya kumpa mtoto ruhusa ya kufanya anachojisikia bila kuzingatia mipaka sahihi inayomuhusu, na aina hii ya malezi inajulikana kama malezi ya kuruhusu.
Haya malezi hayana tofauti na malezi ya kudekeza ila utafauti wake ni kuwa katika haya malezi mzazi anakuwa na huruma kupitiliza ( too much ). Haya malezi yanampa mtoto uhuru uliopitiliza.
Ni malezi yanayomuandaa mtoto kutoweza kuwajibika na kukabiliana na maisha yake ya sasa na ya baadaye, hatoweza kushika majukumu yake yeye mwenyewe na hii hupelekea watoto hawa kutofanya vizuri darasani.
Maisha ya mtoto yanatakiwa yawekewe mfumo na si kumdekeza

Utajuaje kama wewe unawalea watoto wako kwa kuwadekeza!!!
  • Kumuacha mtoto huru kufanya maamuzi mengi mapema kabla ya wakati sahihi. Watoto wadogo hawatakiwi kufanya maamuzi yao wenyewe bila muongozo kutoka kwa mzazi. Mtoto haruhusiwi kufanya kitu chochote bila kuwa na ruhusa yako. Mtoto hatakiwi kupewa kila anachokitaka bali kile anachokihitaji
Malezi ya kudekeza yanamuharibu mtoto
Malezi ya kudekezwa hutafsiriwa vibaya na kuchanganywa na upendo. Ni makosa kuwapa watoto upendo usio na sura ya upendo ( Kuwadekeza ) kama mtoto mdogo wa shule ya msingi kumpa simu, huu siyo upendo ila ni kumuangamiza japokuwa unaonekana kama ni upendo kwa mzazi.
Ni makosa kwa mtoto mdogo kumpa hela na kumzoesha kushika hela. Mkemee mtoto pale anapostahili maana kwa kufanya hivyo utakuwa unamjenga na si kumdekeza kwa maana utakuwa unamuharibu. Usimlee mtoto kama yai bali unatakiwa umuadhibu pale anapokosea, mpe nidhamu inayomuhusu na usimnyime fimbo.
Ukifanikiwa kutumia fimbo ya mti utotoni utatumia fimbo ya mdomo ukubwani. Malezi ya kudekeza yanamfanya mtoto kuwa kama yai

3. MTINDO WA MALEZI YA KUTELEKEZA ( UNINVOLVED PARENTING )
Huu ni mtindo wa kuzaa watoto na kuwatelekeza kwa wazazi au ndugu bila kuwahudumia

4. MALEZI MUAFAKA  ( AUTHORITATIVE PARENTING )
Haya ni malezi yaliyobalance kwa sababu wazazi pamoja ya kuwa wakali wanakuwa na upendo kwa watoto wao. Ni wakali kwa mambo maovu yasiyowafaa watoto wao, lakini pia wana upendo nao pamoja na furaha kutawala katika familia. Na huu ndo upendo unaotakiwa kwa watoto maana ndiyo unaowajenga kitabia na kuja kuwa watu wazuri hapo baadaye.

Pia ni muhimu sana kutambua haiba yako, kama haukusoma somo juu ya kuitambua haiba yako bonyeza link hii ili uweze kusoma
http://mpekesuccess.blogspot.com/2017/09/itambue-haiba-yako.html?m=0#more

0 comments:

Post a Comment

 
Top