Vyovyote haiba yako ilivyo na kwa vyovyote unavyowachukulia wale wenye tabia ngumu fahamu kuwa mfano huo ulishakuwepo miaka mingi iliyopita, labda zaidi ukiwa mtoto ndio ilikuwa chanzo cha vile ulivyo leo; Mwanasaikolojia mmoja aliuita mfumo huu “A child is a father of a man” yaani
Mambo tunayoyaona au unayoyaona kwa mtoto hutupa picha halisi ya ukumbwa wake utakavyokuwa. Zaidi ya asilimia sitini ya yote yanayoendelea maishani mwetu leo yanachangiwa na makuzi yetu tukiwa watoto. Wengi wetu tumejiharibia misingi yetu ya uwezo wa kuishi na watu wenye tabia ngumu na hivyo kujikuta tunaumizwa tokea tukiwa watoto wadogo. Habari njema ni kwamba hakuna ulazima wa kubaki vile ulivyo, mabadilko yanawezakana, inawekana katika hatua yoyote kubadili mtazamo au muonekano wako na kuboresha ujasiri wako.
Tujaribu kuangalia baadhi ya sababu zinazosababisha mtu kujiona au kujitazama vibaya, hii itakuwezesha wewe kujua uko wapi na kwanini.
1. Watu wa kwanza kabisa waliowahi kuwa karibu na wewe ni baba na mama yako au yoyote aliyechukua nafasi yao, mfano mlezi, babu, bibi nk. Kutokana na mtazamo wao juu yako, hapo wewe umetengeneza au kuzalisha mtazamo juu yako mwenywe najinsi unavyojithamini au kutojithamini. Kwa lugha rahisi ni kwamba, jinsi unavyojiangalia ulivyo leo kunatokana kwa kiasi kikubwa na jinsi wao walivyokuwa wanakutazama, kama walikuona wewe lofa na mjinga basi kuna uwezekano mkubwa na wewe leo utajiona lofa tu.

Najua wapo wazazi wasio na hekima wala wema kwa watoto wao, huwasababishia watoto wao majeraha ya kimwili, kihisia na hata kiakili, uzuri ni kwamba fungu la wazazi hawa ni dogo. Ingawa inawezekana sana kwa wazazi au walezi au watu wazima wowote kusababisha majeraha na athari kwa watoto mara nyingine pasipo kujua kwamba wanafanya hivyo. Na mara nyingine watoto wameharibiwa na wazazi wao wenyewe pasipo wazazi hawa kujua kuwa wanawaharibu watoto wao.
2. Wazazi ambao huwalinda na kuwatetea sana watoto wao, wakijaribu kuwafanyia kila kitu kwa niaba ya watoto hao, kwa njia hii wazazi hawa hutengeneza watu wazima (wababa au wamama) wenye utegemezi mkubwa, wasioweza kufanya kitu chochote wenyewe wala kusimama kwa miguu yao wenyewe. Unakuta hata kazi za shuleni mama ndiyo anafanya, mtoto anakuwa hata kuosha mwili wake hajui, na hawa ndio wale ambao ndoa huwashinda mapemaaa.
3. Wale wazazi au walezi ambao hutoa mahitaji kwa watoto wao lakini hushindwa kuonyesha kwa matendo upendo wao kwa watoto wao (mfano. Kuongea nao, kucheka nao, kucheza nao n.k.) hutengeneza kizazi kinachoamini kuwa hakipendeki, hakina mvuto, kisicho na thamani na kisichostahili kupendwa. Baba haijalishi unatoa mahitaji yote yanayohitajika nyumbani kwako, hilo sio pekee watoto wako wanalolihitaji kutoka kwako, wape muda wakuwa pamoja nao, wawehuru kucheza na wewe kidogo, toka pamoja nao, jibu baadhi ya maswali yao, waruhusu kujuwa kumbe baba au mama anaweza kuwakaribu na sisi pia.
4. Wazazi au walezi ambao kila mara humwekea mazingia mtoto kujiona aliyeshindwa, kila wakati ni wakufeli tu, wazazi hawa ni wale wanaosema kwa nini mtoto asijitahidi, kwanini asiwe wa kwanza darasani, ni mpumbavu n.k.. hali hii huharibu kabisa imani ya mtoto kwake yeye mwenyewe, huua kule kujiamini kwake na pia kutokiamini kile anachokifanya.
Yawezekana kuna vitu vilivyoonekana katika makuzi ya mtoto ambavyo hakuna wa kulaumiwa lakini bado vitu hivi huathiri sana kujiamini na kujithamini kwa mtoto yule.
Mtoto au watoto wanaohama hama au kuhamishwa shule mara kwa mara, kwa sababu zao binafsi au kwa sababu ya kuhama hama kwa wazazi hupata shida yakujiona wapweke kwa maana kila wakati hupata kazi ya kutengeneza marafiki wapya na kwamuda fulani hali hii huathiri haiba zao na kujenga kitu tunachokiita “inferiority complex”.

Baada ya kufahamu utofauti mkubwa tulionao kwenye haiba “personalities” zetu, sasa nina jibu swali “Tufanye nini??”
Kitu cha kwanza ni kukubaliana na ukweli kwamba mtazamo wako (jinsi unavyojitazama) hubadilika badilika. Tena hubadilika kiasi ambacho mara nyingine huwezi kutambua. Unaweza kuchagua mwenyewe jinsi unavyotaka mtazamo wako uwe. Kwa mfano;
1. Kufanikiwa au kushindwa
Jaribu kutoangalia nyuma kule ulikowahi kushindwa zaidi, kila mtu anahistoria ya kushindwa sio wewe tu. Wacheza mpira maarufu duniani, mara nyingine hukosa magoli rahisi kabisa lakini hakuna hata mmoja aliye acha kucheza au kuharibu fani yake kwa sababu ya kukosa goli. Wala hakuna aliyekiri kuwa yeye sio bora kwa sababu tu ya kukosa goli moja. Ni vema kukumbuka kule tulikowahi kushindwa kama tu tunataka kujifunza katika makosa yetu, na sio kwa kutaka kujisononesha na kujilaumu kwa namna tulivyokosea. Jifunze kuziacha historia za kufeli na kushindwa zifukiwe katika yaliyopita.

Tengeneza mafanikio yako wewe mwenyewe anza katika hali ya chini kabisa, chagua vile vitu usivyo viweza kabisa kuvifanya mfano; Kuzungumza mbele ya watu, kuimba, kuogelea, kuwa kwenye usaili, kusimama mbele ya kamera n.k anza kuvifanya kwanza kupitia ufahamu wako (viwaze akilini) hali hii inaitwa (creative visualization) ni njia majawapo bora ya kufanya mazoezi ya vile tunavyoshindwa katika fikra zetu, kwanza jitahidi kujitazama fikrani ukiwa au ukifanya vitu hivyo kwa ushindi hadi ufahamu wako utakapoizoea hali hiyo na kuacha kutuma jumbe za kushtuka (kupanick) au uwoga wakati utakapokuwa unafanya vitu vile kihalisi.
Katika kufanya mazoezi ya kufikiria kimtazamo, chagua kufanya katika utulivu mchana au jioni. Muda kabla hujaenda kulala ni mzuri zaidi. Rudia zoezi hili mara kwa mara mpaka uzoee na fikra zizoee.
2. Andika vile vitu uvipendavyo juu yako wewe mwenyewe
Kama kuna mtu anayesema kuwa hana kitu cha kuandika basi mtuhuyo hajafikiri kwa undani au ni mwongo, kila mtu anakitu chema ndani yake.
Kama ukishaandika vitu hivi, angalia tabia ya vile vitu ulivyoviandika pale, kama vitu hivyo vikifanywa na mtu baki usiyemjua je utasema yeye ni mtu mbaya? Kama sio, kwa nini wewe unajiona usiyefaa na uliyejaa mabaya tu?
Badala ya kutazama yale yaliyo mabaya na yakushindwa katika historia yako tazama mafanikio yako. Kila mmoja ana mafanikio ya aina fulani, hata kama ni madogo kiasi gani. Hata kama unatazama yale yaliyowahi kufanyika huko awali basi yatazame katika mtazamo chanya.

Wengi wetu hatuchukui muda kujiuliza vyanzo vya mitazamo yetu hasi, tunaamua kuikubali tu na kuikumbatia na kuifanya asili yetu. Ila mara tu utakapo gundua kuwa tatizo sio lako wewe bali ni mazingira uliyokuziwa au aina ya wazazi uliokuwa nao basi utaacha kujidharau.
Wako watoto wanaofurahia kupelekwa shule za bweni mbali na nyumbani, ila wako ambao hawapendi kabisa lakini wanalazimishwa, hali hii hupandikiza ndani ya watoto hawa upweke, hofu, msongo wa mawazo na kutokutulia (nazungumzia utulivu wa ndani) jambo ambalo huendelea hata katika utu uzima wao. Wako wengi ambao tabia zao za leo zilianza kuharibikia katika shule za bweni mbali na wazazi kwa mfano tabia za kusagana au kuingiliana kinyume na maumbile.

Sisi tumeumbwa katika mifumo na vipindi mbalimbali, mara nyingine tuko chanya (watu wema, wazuri) na mara nyingine tunakuwa hasi (watu wabaya). Kama mtoto atakuwa akiambiwa kila wakati kuwa “kamwe huwezi kuwa na akili kama dada yako” maneno haya hufanyika halisi kwake. Je hujawahi kusikia mtu akisema “mimi sijui kuogelea”, “mimi sijui kama nitaolewa” “Kamwe sitokaa niendeshe gari” , “Mimi sintokaa nijue kiingereza”, “Mimi na kuimba ni tofauti” Haimaanishi kama watu hawa wangeanza kujifunza au kuzaliwa katika mazingira ya vitu hivi, wangevishindwa. Labda kuna sehemu mtu au watu fulani waliwasemea kutoweza au kushindwa na huo ukawa mwanzo wa kuwekewa kizingiti cha ujuzi ndani yao.
Wakati wowote mtu anapojisemea jambo, au neno lililo baya, lisilojenga, lakushindwa, kama utalisema kwa sauti au utalifikiria akilini, katika hali yoyote ile jambo hili hulazimisha uhalisi wa maneno yale kuingia katika mfumo wa maisha yako na kutenda kazi kwa hiyo jifunze kukataa, kukanusha na jitahidi kutenda kinyume na zile sentensi mbaya juu yako. Kama tunaamini utendaji wa kazi wa yale tunayojisemea au kusemewa vibaya basi hata yale tunavyojisemea au kusemewa vema hutenda kazi pia. “If negative proclamation works, surely positive proclamation must work too” Amua kubadilisha yale unayojisema au yale unayosemewa. Badili yale yaliyo negative (yakufeli) yawe positive (yakuweza). Kama hujiamini wewe mwenyewe wala hujithamini, basi utakubali kirahisi kila neno gumu na baya utakaloambiwa na kila mwenye tabia ngumu na kama utayakubali unayoambiwa au unayorushiwa hutaweza kamwe kukabiliana na ushindani kutoka kwa mtu au watu wenye tabia ngumu. Kumbuka daima udhaifu huanzia kwako mwenyewe.
Ukishajifunza kupunguza kujilaumu na kujipinga mwenyewe na kuboresha jinsi unavyojitazama basi utakuwa salama katika kukabiliana na maneno na matendo magumu toka kwa yeyote mwenye tabia ngumu. Na kwa kuwa umejifunza vizuri kujielewa basi sasa waweza kuwaelewa vizuri zaidi wale wenye tabia ngumu. Sasa utaweza kuelewa kuwa kuna kitu kimemfanya au kimewafanya wawe vile walivyo. Mara utakapoweza kumwonea huruma yeyote, haijalishi anatisha kiasi gani basi hawezi tena kukuathiri kwa vyovyote vile.
Kwa jinsi ujasiri wako unavyoongezeka, unaweza pia kuziweka katika matendo mbinu nyingine nyingi za kushuhulika na watu wenye tabia ngumu. Utajikuta unaweza kukabiliana nao na pia kuchukuliana nao katika mazingira tofauti na pia hata katika nyakati ambazo hutakuwa unafanya vizuri katika jambo fulani, hautajilaumu na kujishusha, bali utajisifu kwa kukazana na kujitahidi hata kama haukubahatika.
Uwe na tafakari njema ya makara hii.
Uwe na tafakari njema ya makara hii.
0 comments:
Post a Comment