Katika maisha ni vitu vingi sana ambavyo tunapitia na pengine vinafanya tutengeneze tabia mpya ndani yetu. Swali, Je ni kweli sisi ndivyo tulivyo? Hapana hatutakiwi kuruhusu kila kitu kiweze kubadili tabia zetu ila tunatakiwa kubadilika kutokana na mazingira. Usiruhusu marafiki wabaya wakaharibu tabia yako nzuri, ila ruhusu marafiki wazuri waweze kuimarisha na kujenga tabia nzuri ndani yako. Usiruhusu shida au matatizo kuweza kuharibu tabia yako bali yawe ndo sababu ya kuimarisha tabia yako ya kutokukata tamaa na kuendelea kumtegemea Mungu zaidi.

Usipende kuigiza maisha na kuiga wengine wanavyoishi maana hujui ni vitu vingapi wanavyokutana navyo mpaka wapo vile walivyo. Cha msingi wewe unachotakiwa ni kujifunza kutoka kwao ili uweze kuishi maisha ta uhalisia. Usiruhusu Dunia ikuendeshe bali unatakiwa uendane nayo kutokana na vile jinsi wewe ulivyo ila cha msingi zaidi hautakiwi kuachwa nyuma na utandawazi ( Technology ).
Kwa nini utandawazi? Ni kwa sababu hakuna kitu sasa hivi unaweza kufanya usihusishe utandawazi

Ni matumaini yangu umejifunza kitu hapa hata kama ni kidogo unatakiwa katika kidogo hicho hicho uweze kukifanyia kazi. 

0 comments:

Post a Comment

 
Top