Wataalamu wa mambo ya Saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne nayo ni MELANCOLIN, SANGUINE, COLERICK na FLAGMETIC. Ila kwa leo nitaongelea haiba mbili ambazo zinafahamika zaidi ( common kwa watu ) nazo ni Sanguine na Melancolin
1. MELANCOLIN
- Hawa ni watu wenye uwezo mkubwa sana darasani ( High Intelligence Quotient ), watu ambao wakiamua kufanya jambo wameamua.
- Pia ni watu wasio na maneno mengi, wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati.
- Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo.
- Ni watu wanaopenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao.
- Ni watu wasiopenda kuchangamana.
- Wanapenda kusoma vitabu.
- Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi na ni kundi lenye marafiki wachache.
- Ni wagumu wa kusahau na kusamehe ( Wanaweka vitu moyoni na kuwa uchungu )
-Wanajeruhika mioyo yao kirahisi.
- Ni kundi mojawapo linaloathiriwa na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana.
Katika familia baba na mama wote wakiwa melankolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu watu wa haiba hii si wepesi wa kuadhibu. Na pia watu wa haiba hii hawafai kuwa viongozi kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo kujikuta wanayumba kimsimamo
2. SANGUINE
- Wana uwezo wa kawaida kiakili.
- Ni wacheshi sana na ni watu walio na maneno mengi, wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wanaongea na wengine wanawasikiliza.
- Wanapenda sana kusifiwa. Pia ni wazuri sana katika kusifia.
- Hupata marafiki wengi na kuwa maarufu
- Ni watu wa miemko na hisia, wanaendeshwa na hisia/miemko katika kufanya mambo.
- Wanapenda sana kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine, wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya.
- Ni kundi linaloathiriwa sana na love affairs kwa sababu wana ushawishi mkubwa.
- Ni kundi la watu waoga sana ( wanajiamini sana kwa maneno lakini kwa vitendo ni kunguru )
- Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala.
- Ni watu wenye hasira za haraka na ukiwakosea wanakuadhibu hapo hapo.
Bila shaka utakuwa umeshajijua kuwa wewe upo katika kundi gani kati ya haya makundi tuliyoyaongelea.
Ikumbukwe: Hizi haiba ni tabia ambazo mtu anazaliwa nazo na zipo katika damu.
Kusoma sehemu ya pili ya hili somo ingia hapa http://mpekestn.blogspot.com/2018/01/itambue-haiba-yako-2.html?m=1
0 comments:
Post a Comment