BOMU la nyuklia ni silaha inayosababisha mlipuko mkubwa sana na ni silaha hatari na yenye nguvu kuliko silaha yoyote iliyowahi kupatwa kutengenezwa katika historia ya silaha duniani.
Mabomu haya ya atomia hutengenezwa kwa kutumia madini yaitwayo uraniamu au plutoni.
Pindi lipigwapo bomu hilo husababisha kuondoa kila inachokikuta katika uso wa dunia na kugeuza eneo hilo na kuwa jangwa.

Teknolojia ya kufyatua mabomu ya nyuklia
Kuna namna mbili za kufikisha mabomu haya panapolengwa njia ya kwanza ni kutumia ndege za kivita na njia ya pili ni kutumia roketi. Pia kuna mabomu madogo yanayoingizwa katika makombora ya mizinga.

Nchi ya Japani leo Agosti 6, haitaweza kusahau tukio la kupigwa bomu la Nyuklia katika miji yake ya Hiroshima na Nagasaki ikiwa ni vita ya pili ya dunia ikielekea kufika mwisho.
Japani ilijikuta ikipata kipigo hicho kitakatifu kutoka kwa Marekani ambayo iliamriwa kufanya hivyo na rais wake Harry S. Truman, kupiga mabomu hayo mfululizo kutokea Agosti 6 hadi Agosti 9, 1945.
Bomu hilo ambalo lilipewa jina la ‘Little Boy’ liliporomoshwa jiji la Hiroshima siku ya jumatatu, Agosti 6, 1945, hadi Agosti 9, 1945 likamaliziwa na mji wa Nagasaki na kuandika historia ambayo haitasahaulika duniani.
Mlipuko huo hasa ndiyo uliosababisha kupinga utengenezaji wa mabomu ya aina hiyo kwani ulifanya maangamizi makubwa kwa kuua jumla ya watu 140,000 huko Hiroshima na 80,000 wa Nagasaki mwishoni mwa mwaka 1945.
Siku chache baada ya kumalizika kwa tukio hilo inakisiwa kuna asilimia kati ya 15 na 20 ya watu waliopoteza maisha kutokana na majeraha waliyoyapata kutokana na bomu hilo.
Wapo waliofariki kutokana na hewa ambayo ilikuwa ya sumu kutoka katika bomu hilo, wengine walikufa kutokana na mionzi yake na wengine kupata kansa.
Kutokana na uwezo wa mabomu hayo siku sita ya kupigwa kwake huko Nagasaki, Agosti 15, Japani ilisalimu amri na Septemba 2 alisaini kuachana na vita hivyo.
Mji huu wa Hiroshima ulijengwa upya baada ya vita kuu ya pili ya dunia kumalizika. Katika mji huu kuna gofu ambalo linajulikana kama ‘Kuba ya Bomu ya nyuklia’ ni gofu la nyumba lililohifadhiwa kama kumbukumbu ya mlipuko, na jengo hilo limeingizwa katika orodha ya urithi wa dunia.
Kabla ya kushambuliwa kwa mji huu, ulikuwa na msongamano wa watu waliokuwa wakifikia 381,000 lakini baada ya vita kuisha idadi hiyo ilipungua na kufikia kiasi cha watu 255,000.
Mji mwingine uliokumbwa na shambulio la mabomu hayo ulikuwa Nagasaki ambao nao unapatikana katika kisiwa cha Kyushu.
Mji huu nao umejizolea umaarufu kutokana na shambulio hilo la mwaka 1945 na kwa sasa unatumiwa kama mji wa pili wa kihistoria baada ya Hiroshima.
Mji huu ulipopigwa na bomu ulisababisha mauaji ya watu 36,000 hapo hapo na wengine waliokadiriwa kuwa kati ya 70,000 na 100,000 kufariki baadaye kutokana na maradhi yaliyotokana na nyuklia.
Inadaiwa kwamba baada ya kupigwa bomu hilo iliathiri mfumo wa mawasiliano na kituo cha redio kilikata kurusha matangazo yake kwa muda wa dakika 20 ikiwa ni pamoja na usafiri wa reli kuacha kuingia katika mji Hiroshima kwa umbali wa kilomita 16.
Nchi ya Japan iliingia hasara kubwa ikiwamo upungufu wa dawa kutokana na watu wengi kuathirika na mabomu hayo.
Wapo watoto waliokuwa wakizaliwa kiajabu wengine wakizaliwa wameungana, na inakadiliwa mwaka 1950 na 1990, asilimia 9 ya watu waliathiliwa na ugonjwa wa kansa na mkanda wa jeshi.

Wataalamu miaka ya 1980 waligundua kwamba iwapo milipuko hiyo ingelipuliwa kwa robo hadi nusu ya silaha za nyuklia zilizokuwepo tayari ingetosha kumaliza maisha ya dunia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ingetokea.
Maradhi haya yangesababishwa kwa kiasi kikubwa na vumbi iliyokuwa ikirushwa hewani na milipuko hiyo ya wakati huo.
Inadaiwa kwamba vumbi hiyo ingejaza anga na kuzuia nuru ya jua kufika kwenye uso wa dunia hivyo kusababisha giza pamoja na kushuka kwa halijoto kwa muda wa miaka kadhaa.
Katika vita hii waliokufa hawakuwa wajapan pekee bali pia wakorea wapatao 20,000 walifariki huko Hiroshima na wengine 2,000 walifariki katika mlipuko wa Nagasaki.

0 comments:

Post a Comment

 
Top