Miaka 21
iliyopita nilifunga ndoa na mume wangu mpendwa kanisani, baadaye tukajaliwa
kuwa na watoto wawili mmoja wa kiume Alfred na mwingine wa kike Minza. Mimi
nimesomea mambo ya uuguzi MD, nimefanya kazi muda mrefu ktk hospitali za
wilayani karatu na Arusha mjini mpk nilipolazimika kuacha kutokana na udhaifu
wa mwili na mambo yaliyonipata katika maisha. Mume wangu alikua ni askari
polisi mpk baadaye alipojiunga na ajira zingine mpaka alipokutwa na mauti kama
nitakavyoeleza baadaye hapo chini.
Tulipooana na
mume wangu,maisha yalikua ya furaha sana na tulikua na mipango mingi mizuri ya
kujiendeleza kiuchumi na kihuduma kwani tulikua tunampenda Mungu na tulikua
waimbaji na waombaji kanisani. Baada ya muda mrefu katika maisha ya ndoa na
familia, baadaye maisha yalianza kuwa magumu kutokana na mishahara yetu kuwa
midogo ukilinganisha na mahitaji. Mume wangu alijisikia vibaya sana zaidi yangu
hasa pale alipoona wengine hasa marafiki zake wanafanikiwa lkn yeye hafanikiwi.
Kuna maaskari walikua wakipandishwa vyeo haraka na kuhamishiwa mijini ikiwemo
Dar-es-salaam na Arusha- hali hiyo ilimpa shida sana akawa anaomba na kufunga
kwa muda mrefu lkn hakuona mafanikio.
Wakati fulani
ilitokea akakutana na rafiki yake askari mwenzie, akamualika nyumbani kwake.
Mume wangu aliporudi akaja akiwa mwenye mawazo makubwa sana, sikujua ni kwanini
na hukuniambia hata nilipomuuliza.
Baada ya siku
kadhaa mume wangu akaacha kwenda kanisani wala huduma hakufurahia tena. Akawa
ni mkimya na mwenye mawazo mengi sana. Siku moja akaniambia atasafiri kikazi
kwa muda wa siku tatu. Baada ya siku tatu akarudi akiwa hoi sana na mgonjwa km
mtu mwenye malaria. Nikajaribu kumshawishi twende hospitali hakukubali kbs
akaniambia ni uchuvo tu wa safari na kazi na atakuwa salama. Kesho yake, kweli
akaamka vzr na kwenda kazini bila kuugua km hapo jana. Ikapita muda mrefu bila
kujua hasa nini kinachoendelea kwa mume wangu kwani hakuniambia chochote hata
nilipomuuliza.
Baada ya muda,
mume wangu akapata nafasi ya kwenda masomoni Moshi. Alipomaliza masomo
hayo,haikuchukua muda mrefu tukapata barua ya uhamisho wa mume wangu kikaz
kuelekea Arusha mjini.
Binafsi
nilifurahi sana, nikajua Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya siku nyingi. Kwa
hiyo na mimi nikaanza mipango ya uhamisho. Tulipofika Arusha tukapata makazi
mapya na kanisa zuri la kuabudia. Baada ya muda niligundua mume wangu hakupenda
mambo ya Mungu km siku za zamani. Wakati huu mimi nilikua mjamzito nikijandaa
kupata mtoto wa pili.
Tulizungumza
sana na mwenzangu lkn sikujua hasa kitu gani kilikua kinamsumbua. Baada ya muda
niligundua mume wangu alikua mlevi wa pombe na tabia yake ilibadilika sana hasa
kuhusu mambo ya kiimani na kushirikishana mipango. Aligeuka kuwa mtu wa mambo
mengi, kuamrisha na msiri sana- kutokana na aina ya kazi zao nikajua ni
kawaida.
Nilipojifungua
mtoto wetu wa pili akaniletea zawadi ya gari mark2-mimi nilikua miongoni mwa
wanawake wachache kuendesha mark2 wakati ule miaka ya90 mwishoni. Tulijisikia
vzr sana na mambo ni kama yalikua yananyooka.
Mwaka 2001 mume
wangu alipata nafasi ya kwenda tena chuoni kusoma kwa muda mfupi huko Dar,
nikabaki na familia na nikawa naendelea vzr na kazi zangu. Alipomaliza masomo
akarudi na maisha yakaendelea kwa muda km kawaida. Baada ya miezi kama sita
kutoka chuoni, mume wangu akaniambia anataka kuacha kazi- nilishangaa sana
nikamuuliza maswali mengi lkn hukunijibu vzr. Wiki moja baadaye akaniambia
ameacha kazi na ameajiriwa shirika moja kubwa la UN hapa Arusha.
Kweli akaanza
kuvaa sare mpya za kazi hiyo mpya. Kazi hiyo mpya ilituletea mafanikio makubwa
sana ya kifedha na kujieneza kwa mali. Wakati huo pia mimi nilipata nafasi ya
kwenda kusoma chuoni muhimbili Dar kwa muda wa miaka mitano. Nikaenda Dar
nikaiacha familia ikiendelea vzr kbs.
Nikiwa Dar
chuoni nilipata nafasi ya kwenda nje ya nchi kufanya seminar ya health
exhibitions (mafunzo ya maonesho)- nikiwa huko nilipigiwa simu kuwa mtoto wetu
mdogo amefariki dunia. Nilichanganyikiwa nikarudi nyumbani kwa kuchelewa,
nikakuta wameshamzika Alfred mwanangu sikumuona tena. Ilisemekana alifariki
ghafla sana bila kujua hasa ni ugonjwa gani au alipatwa na nini mwanangu.
Niliongea na madaktari, wakanieleza kuwa mwanangu alitokwa na damu nyingi sana
mpk ndani ya jeneza. Uchungu mkubwa na kuchanganyikiwa vilinipata bila kujua
hasa nini cha kufanya.
Niliporudi
msibani nilishangaa kumkuta mume wangu akiwa na pete kubwa ya dhahabu yenye
kinakshi cha tanzanite katikati ya mkono wa kuume. Nilipomuuliza akaniambia
amenunua mjini bei ghali sana na pia ameninulia na mimi aina kama hiyo ya pete.
Sikujua chochote nikaipokea ile pete kama zawadi nikawa naivaa. Pia akaniambia
kuna kanisa jipya limeanzishwa hapa mjini ndio tutakua tunasali. Huko
tulikutana na watu mbalimbali wa mataifa mengine na ibada zilikua ni za
kiingereza. Tulienda kutambulishwa na mume wangu kwa mchungaji ambaye nayepia
alikua amevaa pete kama ya mume wangu-sikujali sana kwa siku hiyo. Nilijisikia
vzr sana kwani huko nilimuona mume wangu akifurahia na kujitoa kama zamani. Pia
tulipata marafiki wengi akiwemo familia moja ya wakameruni waliokua karibu sana
na sisi. Tukahamia huko.
Baada ya muda
baada ya kuipata ile pete na kurudi chuoni na kujiunga kanisa jipya huku
Arusha, sikupenda tena kwenda kanisani wala kujishughulisha na mambo ya huduma
kama awali. Nilijiona mwenye majukumu mengi sana na sina muda wa mambo ya
kanisani na huduma. Wenzangu waliponiuliza, niliwajibu kuwa niko bize sana na
masomo na shughuli za kikazi. Nikawa mzembe sana ktk mambo ya imani na huduma.
Lkn siku moja
Nikiwa Dar wakati wa fellowship za chuoni, ndugu mmoja alitutembelea akahubiri
kwa nguvu sana akatuambia kuna mtu amezingirwa na roho mbaya za kichawi
zinazotafuta kumuangamiza na familia yake-sikuelewa hata kidogo wala hakupita
mtu yeyote mbele siku hiyo. Yule muhuburi alilia sana kwa uchungu mpk mwisho wa
ibada.
Baada ya kumaliza
masomo mwaka 2007 nilirudi Arusha. Nikapata marafiki wengi na mitandao
mbalimbali ya kibiashara ndani na nje ya nchi. Pesa ilikuwa nyingi mpaka
nikashangaa kuwa ni baraka za namna gani.
Mwaka 2009 siku
moja nilishtuka na kitu kimoja pale mume wangu aliposahau pete yake (ile
nyingine anayovaa mkono wa kuume sio ya ndoa) nyumbani. Mimi bila kujua
nilipoiona niliihifadhi kwenye mkoba wangu nikaondoka nayo. Kumbe nyuma yangu,
mume wangu alirudi nyumbani ghafla na kuitafuta sana pete akanipigia simu
nikamwambia ninayo kwenye mkoba aje nilipo aichukue. Cha ajabu alipokuja ili
nimpe ile pete haikuwepo tena kwenye mkoba. Nilijikagua na kuwauliza wafanyakzi
wenzangu lkn pete haikuonekana. Mume wangu alichanganyikiwa na kunishambulia
kwa makofi na matusi akiwa mwenye hasira kubwa- sikuwahi kumuona mume wangu
akiwa mwenye hasira na ghadhabu kubwa
kiasi kile. Alinidhalilisha hadharani mbele ya wafanyakazi wenzangu na
kuniamrisha twende nyumbn haraka. Ofisi yao ilikua nikaribu na ofisini kwangu
lkn alinipandisha gari yake na tukaelekea nyumbn bila kupitia ofisini kwao.
Kwenye gari tulikua tunagombezana kwani nilijisikia kudhalilishwa kwa hali ya
juu sana.
Tulipofika
nyumbani, ugomvi ulikua mkubwa sana na sana mume wangu alinipiga kweli. Baadaye
watu walikuja lkn hawakuweza kuingia ndani kwani kulikua kumefungwa. Mume wangu
alinifungia kwenye chumba kimoja na nikamsikia akiwapigia simu watu kadhaa huku
akilia km mtoto. Sikuelewa kwa kweli. Mchungaji wa kule kwenye kanisa letu
alikuja na mtu mmoja ambaye alikua ni rafiki wa karibu wa familia yetu lkn
foreigner.
Walipofika
waliongea na mume wangu kwa muda afu wakaondoka. Mume wangu akaja akanifungulia
mlango akaniambia tuongee- wakati huo alikua mpole na mkimya asiyelia tena.
Akaniambia kuwa
ile pete iliyopotea ilikua ndio pete ya maisha yetu. Alipewa na huyo mchungaji
na ilikua inamasharti makubwa kuwa lazima aivae yeye tu na isikae muda mrefu
nje ya kidole chake. Kwa ufupi pete hiyo haikuwa ya kawaida na ile pete ilikua
ni yule mtoto wetu (Alfred) aliyekufa miaka kadhaa iliyopita. Nilishtuka kujua
hata ile pete niliopewa mimi haikuwepo mkononi mwangu wakati huo. Ilikua
imetoweka, nikazimia kusikia maneno hayo. Nilipozinduka nilijikuta nyumbn kwa
mchungaji nikiwa nimelazwa kitandani. Kumbe nilipozimia nilipelekwa hospitali
na pia mume wangu akakamatwa na polisi akawekwa lokap lkn akaachiwa baadaye
kutokana na ushawishi wake pale polisi na alipowaelezea anavyojua yeye.
Alipotoka akaja hospitali wakanichukua mpk nyumbn kwa mchungaji. Nilipozinduka
nikamuona mchungaji na yule rafiki yetu mkameruni walikua wamevaa pete km ile
ya mume wangu iliyopotea. Hawakunisemesha kitu wala hawa kuomba lkn waliondoka
kule chumbani wakiniacha na mume wangu mara baada ya kupata ufahamu.
Mume wangu
alinichukua mpk nyumbn, tulipofika hatukuongea kitu mpk asbh. Yeye alienda
mjini baadaye akarudi akiwa bado mwenye mawazo na wasiwasi mkubwa. Siku hiyo
ikapita na kesho yake. Marafiki zangu walikuja kunitembelea ili kunipa pole lkn
hawakuruhusiwa. Kumbe mume wangu aliwaambia watu pamoja na ndugu zangu kuwa
nimemuibia mali nyingi sana nimeficha kusikojulikana. Ndugu zangu walipokuja
aliwaruhusu kwa masharti kuwa nisiwaambie ukweli. Akanitisha kuwa nikisema
ukweli tutakufa wote.
Maisha yaliendelea kwa siku kadhaa,
nikaendelea na kazi lkn nikiwa mwenye mawazo makubwa. Nikaomba off kazini kwa
muda ili nipate ahueni. Mume wangu naye akaomba off pia tukawa tunashinda ndani
tu. Nyakati za usiku nikiwa nimelala mara nyingi niliota ndoto kuwa Alfred
mwanangu ananiita yuko barabarani anahangaika akiwa analia. Nikimwambia mume
wangu ananiuliza ni wapi eneo gani hasa, nikimtajia eneo nilipoota ananiambia
hapo ndipo pete ilipo kwa hiyo ataifuata- nakweli mara nyingi alikua anaamka
anaondoka eti kuifuata hilo eneo nilipomuona mtoto wangu kwenye ndoto.
Pete ile
haikuwahi kuonekana na maisha yetu yalianza kuporomoka siku hadi siku. Mume
wangu hakufurahi tena. Alikua ni mtu mwenye majonzi na wasiwasi sana juu ya
maisha yetu siku zijazo. Wakati huo aliwafukuza wafanyakazi wote wa nyumbn na
alininyanganya simu zote na alifungia ndani nisitoke nje
Siku moja
ikitokea mjini katika mizunguko yake alinijia na habari mpya akidai kuwa ndio
suluhisho la tatizo letu. Aliniambia kuwa ili turejee ktk maisha yetu ya
kawaida inabidi tumuue mtoto wetu Minza pia kwa siku zote za maisha yetu
kuanzia siku hiyo itakua ni marufuku kufanya mapenzi kwa njia ya kawaida ila tu
kinyume na maumbile (yaani awe ananiingilia kinyume na maumbile ya mwanamke).
Akaniambia hakuna namna nyingine ya kurejesha maisha yetu zaidi ya hivyo. Nilishtuka
sana nikaogopa mno. Nilimlaumu sana mume wangu kwanini alijiingiza ktk maisha
hayo- ndipo akanieleza habari kamili kuwa mafanikio yetu yote yametokana na
mfumo huo wa maisha tangu siku ile aliporudi ile safari tukiwa Karatu. Kumbe
siku ile alikua ametoka kwa mganga aliyepelekwa na yule rafiki yake.
Nilimshauri mume
wangu twende kwa mchungaji tukaombewe lkn akasema kuwa tukisema tu kwa watu
tutakufa wote. Pia akasisitiza kuwa sisi wote tuko katika mtandao huo kwa hiyo
sio rahisi kujiokoa tena. Kesho yake mume wangu alinikumbushia tena akasema ni
lazima tufanye hivyo na pia sio kwa kulazimisha inatakiwa iwe kwa hiari ili
tupate faida kwa haraka. Bado nilikataa, sikuwa tyr kufanya hivyo. Nilimuomba
mungu usiku na mchana atusaidie. Lkn mume wangu Alinitisha sana na kunifinya
mwili ili nikubali kwani alikua mwenye hasira na ghadhabu kubwa. Pia
alinifungia ndani ili nisitoke nje. Pia alisisitiza nisiombe kbs. Maisha
yaligeuka kuwa jehanam.
Siku kama mbili
zililizofuata tulipigiwa simu kutoka shuleni kwao na mtoto wetu kuwa Minza
ametoweka shuleni hajulikani alipo. Tulikwenda haraka kujua hatma ya mtoto
wetu. Niliogopa zaidi kwani nilijua labda ndio keshapatikana- japo mume wangu
alionekana kuwa si mwenye wasiwasi hata kidogo. Nilianza kukumbuka kukemea na
kuomba Mungu atusaidie lkn mume wangu alinikataza nisiombe kbs. Akanizabua
kibao kikubwa mdomoni tukiwa kwenye gari mpk damu ikatoka mdomoni. Nikisikia
uchungu mkubwa zaidi kwanini maisha yalikua yanaenda hivyo ghafla au nini faida
ya kuishi basi.
Tulisafiri siku
nzima mpk kufika shuleni kwa Minza mwanangu. Kitu cha ajabu ni kwamba tulimkuta
mtoto akiwa hospitali amelazwa haongei wala hajitambui na taarifa zinasema
alikutwa chumbani(hostel) kwao mchana huo akiwa anatokwa na damu nyingi.
Siku kadhaa baadaye
tulipewa mtoto wetu baada ya kupata nafuu tukarudi naye nyumbani kwa matibabu
zaidi. Minza aliendelea kuugua sana bila nafuu na hakuweza kuzungumza kitu
alikua ni mtu wa kulala kitandani na kutazama tu.
Ilipita miezi
kadhaa maisha hayo yakawa yamechukua sura ya familia yangu. Miradi kadhaa
tuliyoifungua mjini ilikua imefungwa, pia kazini kwangu nilikua nakwenda kwa
shida sana. Uwezo wangu wa akili na kiutendaji ulipooza sana. Nilijiingiza
kwenye chama cha ulevi wa pombe km mume wangu ili kupoteza machungu na kupunguza
mawazo. Lkn hai kusaidia. Lkn kule kanisani tuliendelea kwenda na mume wangu
aliendelea na kazi kule UN.
Siku moja mume
wangu aliniambia tunakwenda shambani kwa siku kadhaa twende wote- tulijiandaa
tulikwenda pamoja. Tulipofika huko, tulijumuika pamoja na mchungaji na yule
rafiki yetu mkameruni. Tulifurahi na kunywa na kula mpk usiku kwa siku hiyo ya
kwanza. Kesho yake asubuhi na mapema niliitwa na mume wangu kuwa kuna kikao-
Cha ajabu ni kwamba asubuhi hiyo mchungaji na yule mkameruni walikua wamevalia
mavazi ya kitamaduni kupitiliza kawaida yao. Tulikwenda mpk vichakani zaidi
kwani walisema kuna maongezi muhimu sana.
Tukiwa huko yule
mchungaji alitueleza waziwazi kuwa yeye ni mtu mwenye nguvu nyingi sana na
amewasaidia wengi sana. Na pia hata zile mali za kwanza na kufanikiwa kwetu ni
yeye ndiye aliyetusaidia kwa nguvu zake. Na nguvu hizo zilitokana na pete yake.
Pete yake ndio inayompa nguvu na kumletea bahati na mvuto kwa watu.
Kwa kuwa tulikua
tumeshindwa kutekeleza sharti la kwanza la kumuua Minza na muda ulikua umepita
basi, kuna sharti lingine la mwisho
Kwa hiyo,
akasema anao uwezo wa kutupatia pete nyingine lkn ndio kwa masharti. Na leo
hapo yuko tyr kutusaidia tena ili tufanikiwe na tusife- kwani tulikua tumefanya
makosa makubwa sana kupoteza ile pete ya awali.
Akatoa masharti
ili tupate pete nyingine inabidi mimi nikubali pale niingiliwe kimwili nao wote
watatu. (yaani nifanye mapenzi na wote watatu pale kichakani hadharani na mmoja
baada ya mwingine akianza mume wangu). Vinginevyo mume wangu atapoteza maisha
pale pale na mimi pia ningekufa siku zijazo au ningekua kichaa. Nilishtuka
nikaogopa sana, nikaanza kupiga mayowe huku nikikimbia kuelekea kwa mume wangu-
nililia sana kwa uchungu huku nikitaja jina la mume wangu kwa kumlaumu kwanini
alijiingiza kwenye mambo hayo. Mume wangu alinisihi nikubali ili tusife kwani
hakukua na namna nyingine.
Sikukubali.
Nilianza kukimbia kuelekea barabarani kuhofia usalama wangu kwani niligundua
mume wangu hakuwa na uwezo tena wa kunisaidia au kujiokoa. Nilpofika mahala
tulipopaki magari yetu sikuona gari hata moja. Nikiwa ktk hali ya kukimbia na
kujiokoa huku nikipiga mayowe niliwaona yule mchungaji na yule mkameruni
wamenitokea nyuma na mbele yangu. Ghafla yule mchungaji aliniwekea mkono
kichwani nikaanguka chini nikapoteza fahamu.
Niliporejea
fahamu zangu ni siku nilipojikuta niko katikati ya kundi la watu walinisimamia
na kuniangalia kwa umakini mkubwa sana. Kumbe ilikua ni kwenye maombezi. Fahamu
zangu zilinirejea na kujitambua japo nilikua nimeharibika mwili na mavazi
machakavu pia nikiwa nimefungwa kwa kamba ngumu sana. Nilifanikiwa kuwatambua
baadhi ya ndugu jamaa na marafiki waliokuwepo pale.
Kwa masaa kadhaa
nilijisikia kupumbaa kama mjinga bila kujua nifanye nini. Alitokea mtu mmoja
akaniambia pole. Akaniuliza kama ninajisikiaje kwa wakati huo. Nikamuelezea.
Kisha nikamuhoji kuwa hapo ni wapi- akaniambia kuwa ni kituo cha maombezi na
yeye ndiye mchungaji.
Inasemekana kuwa
siku hiyo nilikua nimefunguliwa kutoka katika ukichaa ulionisumbua kama miaka
mitatu na nusu. Katika muda wote huo niliishi msituni kama mnyama. Nilitafutwa
na ndugu zangu kwa muda mrefu sana bila mafanikio. Hakuna mtu alijua mimi au
mume wangu tulikua wapi.
Baadaye
Nilipouliza kuhusu mwanangu Minza na mume wangu, nijibiwa kuwa waliokufa miaka
mitatu na nusu iliyopita. Ndipo nikakumbuka mambo magumu ya maisha
yaliyonipata. Nilitunga msiba mkubwa upya kabisa. Nililia sana na kujionea
huruma kama yatima asiye na msaada. Sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu
kwa yote. Hata uhai nilionao leo ni Mungu tu amenisaidia.
Sasa hivi nipo
tu kwa ndugu zangu tunaishi na maisha yangu mapya ya kumtumaini Mungu wangu kwa
upya kabisa. Bwana Yesu Kristo ndiye msaada wangu wa karibu. Ninamshukuru Mungu
kwa familia yangu mpya ya wana ndugu ndani ya Kristo Yesu. Mungu awabariki.
AMEN.
UJUMBE HUU UMEKUJA KWAKO KWA MAFUNDISHO YA
KIROHO JUU YA IMANI POTOFU ZIHARIBUZO KUSUDI LA MUNGU JUU YA MWANADAMU NA
ULIMWENGU KWA UJUMLA. MWAMINI YESU UPATE UZIMA WA MILELE.
0 comments:
Post a Comment