Morning hope
Jana imepita hatimaye leo ni siku nyingine, kama jana kuna jambo halikwenda vizuri unaweza lirekebisha leo ili kesho yako iwe nzuri zaidi. Usikubali kushindwa na kuwa kama watu waliolala makaburini ambao wamelala na utajiri mkubwa baada ya kushindwa kuutumia pindi walipokuwa wanaishi hapa duniani. Ishi kishujaa, inawezekana bado haujajijua kuwa wewe ni nani, ngoja nikukumbushe kidogo katika Bibilia kitabu cha Mwanzo 1:26, Mungu anasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu, akatawale...
Yah kumbe wewe umeumbwa kuja kutawala na pia umeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu wetu hajawahi kushindwa hivyo basi na wewe usikubali kushindwa. Siku zote penye nia pana njia, usikate tamaa kwa chochote unachokifanya kwa maana ushindi wako upo. Na haijalishi umeshindwa au utashindwa mara ngapi usipoteze matumaini wala usikate tamaa ipo siku utafanikiwa tu katika hilo
Nikutakie tafakari njema na siku njema.
0 comments:
Post a Comment