Habari za wakati huu popote ulipo, ikiwa ni siku ya 4 tangu mwaka 2018 uanze ni mtumaini yangu kuwa unaendelea vizuri. Leo ningependa nikukumbushe juu ya unavyotakiwa kuwa na maono, muonekano wa maono yako
Ukweli ni kwamba ili ufanikiwe katika maisha yako unatakiwa uwe na maono makubwa mpaka uhakikishe yanakusumbua, ikifika asubuhi yakufanye uwahi kuamka kitandani. Yakusukume kufanya kitu pale utakapokuwa umechoka na hayo ndo maono.
Siyo unakuwa na maono ambayo kila mtu anayo kama kuoa na kuolewa, au kuwa na nyumba uwe na familia yako. Hapana, hayo ni maono ambayo kila mtu anayo, unatakiwa uwe na maono mengine tofauti na hayo ambayo yatakuwa ni makubwa zaidi mpaka ukiwaambia watu wasiamini kama unaweza kuyafanya. Na kwa njia hii yatakufanya uweze kufika kwenye mafanikio yako.
Nikutakie tafakari njema.

0 comments:

Post a Comment

 
Top