Unafanya nini ili kuifanikisha kesho yako?
Hili ni swali la msingi ambalo kila mtu anatakiwa ajiulize kila iitwapo leo. Tusijidanganye na hili narudia tena kusema: hakuna mafanikio yanayokuja kwa bahati mbaya, wote waliofanikiwa walifanya kitu kilichowawezesha wao kufanikiwa. Nichukulie mfano unakuta mwanafunzi anasoma anataka kuja kuwa mtu fulani lakini hataki kujifunza juu ya vile anavyotaka kuja kuwa. Kuna mtu mmoja alisema kila baada ya miaka miwili utandawazi unabadilika akiwa ana maana kile unachokuwa umekisoma kinakuwa kime-expire na unatakiwa ujue mbinu nyingine mpya, kama dokta anatumia njia fulani kutibu ugonjwa fulani, baada ya miaka mitano kutakuwa na njia nyingine mpya ya kulitibu hilo tatizo, kwa hiyo ili kuendana na hiyo kasi ya utandawazi dokta anatakiwa kuwa up-dated kwa kujifunza.
Wewe unataka kuja kuwa msanii kwa mfano, je ni mara ngapi unajifunza au kufanya mazoezi juu ya hicho kipaji chako, au unadhani utakuja tu uibuke na kuwa msanii mkubwa bila kujishughulisha, lahasha haitakuwa hivyo.
Unataka kufauru masomo yako darasani, je unasoma kwa bidiii, au wewe kila siku ni movie tu na starehe halafu mwisho wa siku unataka ufauru.
Je ni nini kinachohitajika ili kufanikisha kesho yako!!!
Bidii na uthubutu. Ni bora Ukashindwa baada ya kujaribu kuliko kushindwa kujaribu.
Kama una mawazo ya kuja kuwa na pesa, je unafanya nini ili kupata hiyo pesa, au unadhani hela itakuja kwa kuangalia na kusikiliza motivation kutoka kwa watu kila siku bila kufanya kazi, tubadilikeni jamani.
Wengine wanafikilia ili wao waje kufanikiwa ni mpaka watakapokuja kuwa na elimu nzuri. Ngoja nikuambie ndugu yangu mwenye mawazo kama hayo, si mabaya ila napenda nikukumbushe kuwa fanya survey angalia wale wote waliofanikiwa asilimia nyingi hawajafanikiwa kwa sababu ya kile walichokisomea. Sina maana kama kusoma ni vibaya, lahasha! ila unaposoma unatakiwa uwe na mipango mingine zaidi ya kusoma kama na wewe unataka kuja kuwa miongoni mwa watu watakaofanikiwa kifedha. Tatizo hapa wengi wetu huwa tunajishughulisha na elimu ya darasani na kusahau kuwa kuna elimu nyingine inayoitwa elimu Dunia ambayo hii wengi waliofanikiwa ndiyo wanayoitumia.
Mwingine hapa ukimuambia habari za biashara, atasingizia kuwa hana mtaji, ok nikuulize swali: kwani mtaji wa biashara unaanzia shilingi ngapi?. Wengi wanafikilia hela kubwa kama 500000 au 1000000. Wanasahau kwamba kuna biashara ambazo mtaji wake ni chini ya 100000.
Kuna watu hapa hata uwape milioni 50, bado watakufa masikini ni kwa sababu hawana mipango nayo hiyo hela, watakachojali wao ni kutumia tu utasikia wanasema wanaponda mali kufa kwaja. Huwezi ukangoja ufanye mipango baada ya kupata hela, mara nyingi utaishia kufanya maamuzi ambayo siyo sahihi kwa sababu hukuitegemea hiyo hela. Mfano mzuri chukulia wachimbaji wa madini migodini kawaulize zile hela wanazozipata huwa wanapelekaga wapi.
Nina mengi ya kusema ila nimalizie kwa kusema kuwa, kesho yako inajengwa na wewe mwenyewe, haijengwi na mzazi wala mtu yeyote wa karibu yako. Jishughulishe na kazi zitakazo kusaidia kufikia vile unavyotaka kuwa, usiishie kuwaza tu na kuwa mtu wa kudream big kila siku bila kufanyia kazi kile unachokiota. Kumbuka kuwa, Nahodha wa maisha yako ni wewe mwenyewe
Amen
ReplyDeleteHongera; tembelea hapa uone mambo ya kuepuka maishani https://eliamuginiblogadress.blogspot.com
ReplyDeletehttps://eliamuginiblogadress.blogspot.com
ReplyDeleteHongera; tembelea hapa uone mambo ya kuepuka maishani https://eliamuginiblogadress.blogspot.com
ReplyDelete