Tafakari ya asubuhi
Je ushawahi kuongea kitu mbele za marafiki zako kuhusu mafanikio mpaka wakakucheka wakahisi kuwa ni ndoto! Labda uliwaambia kuwa kwenye maisha yangu nataka nije nimiliki gari la thamani kama Range Rover, Bugat, Lambogin au mengineyo yenye thamani, au ukaawaambia nataka kwenye account yangu kabla sijafa nifikishe zaidi ya bilioni moja. Imeshawahi kukutokea hii kwako! Kama jibu ni ndiyo, usikate tamaa songa mbele na hivi ndo inavyotakiwa. Inabidi uwe na maono ambayo mpaka ukiwaambia watu watashtuka na hayo ndo maono. Cha msingi ni kuyapigania hayo maono yako mpaka uhakikishe unayafikia.
Remember: You are supposed to be extraordinary person and not ordinary person. Think Big
Uwe na tafakari njema na siku njema.
0 comments:
Post a Comment