Napenda sana kujifunza kwa mtoto mdogo hasa hasa kipindi kile anapoanza kutembea, kila akianguka anainuka na kujaribu kutembea tena, hachoki hata akiendelea kuanguka anasimama tena na kuendelea kutembea mpaka mwisho wa siku anajua kutembea. Je wewe upo tayari kuwa kama mtoto mdogo kipindi anapoanza kutembea!!! katika kila kitu unachokifanya iwe ni katika biashara yako, au masomo yako au katika kitu chochote kile unachokifanya. Je ukianguka au kufeli katika lile jambo unalolifanya, upo tayari kusimama na kusonga mbele kama mtoto mdogo afanyavyo pindi anapoanguka? au utaacha kwa kuogopa vicheko kutoka kwa watu pale utakapoanguka tena kwa mara ya pili.!!!
Hey my sister and my brother wake up, kubali kujifunza kutoka kwa mtoto mdogo. Usikubali kushindwa jambo eti tu kwa sababu watu watakucheka, kumbuka hao wanaokucheka nao wameshindwa kwenye mambo yao na ndo maana wanakucheka na wewe ili nawe uweze kushindwa uwe kama wao. 
Tafuta watu watakaokuwa tayari kuambatana na wewe katika safari yako ya mafanikio na mwisho wa siku utafika pale ulipopakusudia. Haijalishi utaanguka au kufeli mara ngapi katika mipango yako, ila kumbuka kila unapoanguka ( au kufeli katika jambo ) pale unapoamka tena unapiga hatua kwenda mbele.

1 comments:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

 
Top