Hivi unajijua kuwa wewe ni nani? Yes it is you!!!
Wewe ni mshindi, wewe ni jasiri, shujaa na pia wewe ni watofauti, hakuna aliye kama wewe, hakuwahi kutokea na hatokuja kutokea kamwe. Usijidharau rafiki yangu eti kisa ulishindwa kile ukajiona wewe hujui, rahasha! kushindwa kwako ilikuwa ni ili ujifunze uweze kujua jambo. Kwenye maisha unatakiwa upambane mpaka point ya mwisho usiishie njiani. Kuna mtu alinifuata akaniambia kuwa amechoka kwa maana kila akijaribu kufanya jambo watu wanamcheka, nikamwambia usijali bali vitumie hivyo vicheko kama hasira ya mafanikio. Ndiyo, kuna muda inabidi ufurahie vicheko unavyovipata kwa maana kama utalia haitakusaidia bali utabaki hapo hapo ulipo.
Wewe pia ni mzuri hautakiwi kukili kushindwa, wazuri wote ni washindi
Pia unapo maliza kusoma ujumbe huu napenda nikukumbushe kuwa wewe umeumbwa kwa mfano wa Mungu na Kamwe Mungu wetu hajawahi kushindwa, kwa nini ukate tamaa? Amka na utambue nafasi yako, usikubali kuburuzwa tu bali tafuta kila namna ili na wewe uweze kuburuza.
Wewe ni kipepeo unaweza kuruka ukafika popote unapopahitaji
0 comments:
Post a Comment