Tuesday, 13 February 2018

Maarifa kutoka katika kitabu cha Releasing Your Potential kilichoandikwa na Dr. Myles


RISE UP MOTIVATION@2018

Raisi Kikwete alipokuwa madarakani alikuwa na msemo unaosema kizuri kula na wenzako, nami pia nimeona si vibaya kama tukishirikishana maarifa haya.
Katika sehemu ya sita ya kitabu cha Dr. Myles anaongelea kitu muhimu sana kuhusiana na kutambua chanzo cha uwezo wako ulionao ambao wengi huwa hawajui na kuwasababishia washindwe kufanya mambo makubwa hapa duniani. Akasema lazima pia utambue uwezo ambao Mungu amekupa (ambaye yeye ndo chanzo cha uwezo alionao kila mtu hapa duniani). Pia ameongelea vitu muhimu sana viwili ambavyo ni imani pamoja na matendo (faith and action)
Kwa mfano nimekupa zawadi ya mti wa maembe (kumbuka nimekupa mti wa maembe na siyo maembe). Halafu mtu akaja kukuuliza: aisee hivi Geofrey amekupa nini? Bila shaka utamjibu na kumuambia kuwa amenipa zawadi ya mti wa maembe, pointi ipo hapa: haujayaona maembe ila kutokana na kukuambia na kuweza kujua kuwa nimekupa mti wa maembe, unamjibu mtu kwa imani zote kwamba huu ni mti wa maembe na nikiupanda utazaa maembe. Pointi nyingine hapa, kumbe kuwa mti wa maembe pekee haitoshi kukufanya upate maembe bali ni mpaka pale utakapoamua kuchukua maamuzi ya kwenda kuupanda ule mti ndipo ukuletee maembe. Hiki ni kitendo..

Aaah kumbe kuwa na imani pekee haitoshi mpaka pale utakapochukua maamuzi juu ya kitu fulani ndipo kitakapokuletea matunda. Kwa wakristo kuna neno katika bibilia linasema kuwa "mtakuwa vichwa na si mkia" Hili neno lipo sahii kabisa, ila je ni kweli watu wote waliloliamini hili neno ni vichwa? Jibu ni hapana, ila utakuwa kichwa mpaka uambatanishe na matendo ya kukufanya uwe kichwa, panga malengo yako na usome kwa bidii ndipo utakapokuja kuwa kichwa.
Vile Vile hata katika maisha yetu ya kila siku katika kila unachoamini kama hakuna matendo ni kazi bure, utaishia kusema tu yule amefanikiwa ana bahati, utasikiliza na kusoma hamasa (motivation) nyingi sana ila hazitakusaidia..

Kwa hiyo rafiki amua sasa katika kila imani ya mafanikio uliyonayo wekea matendo, kama una ndoto ya kuja kuwa mtu maarufu basi fanya kitu/vitu vitakavyokutambulisha na kuwa maarufu. Kama unataka kuja kuishi maisha mazuri na unaamini hivyo, basi fanya kazi za halali zitakazokufanya uwe na maisha mazuri.

Na mara nyingi tumesikia na kuamini kuwa Mungu anatuwazia kuja kuishi maisha mazuri, ni kweli kabisa ndugu yangu Mungu ametupa uwezo mkubwa sana ambao kama tukiutumia vizuri hakika tutaishi maisha yoyote yale tunayotaka kuishi. Ila tukikosa imani (kuamini) na matendo juu ya hii imani tutakufa bila kuishi maisha ambayo tulitakiwa kuishi.

Ikumbukwe kuna msemo unasema *"aliwazalo mjinga ndilo litakalomtokea"*. Umeshawahi kukaa na kujiuliza huu msemo una maana gani! Kama tulivyoona hapo juu kuwa kama imani yako utaiambatanisha na matendo, basi hata kama kitu kiwe ni kikubwa vipi utakifanikisha tu. Vile vile hata kwa huyu mjinga aliyesemwa kwenye huu msemo, huwa anawaza kuferi katika jambo lolote (imani ya kuferi)  hivyo humpelekea kutenda matendo yanayoendana na kuferi juu ya kile anachokiwaza. Mwisho wa siku ndiyo anakuja kuferi.

Kwa ushauri wowote bure wasiliana nami kwa namba 0766531758
Email: www.geofreykyando@gmail.com
©Geofrey Mpeke

No comments:

Post a Comment