Habari za wakati huu, ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya. Leo ningependa tumalizie somo letu la 'Itambue haiba yako' ikiwa ni sehemu ya pili. Twende tukajifunze aina mbili zilizobakia za haiba ambazo ni Flagmetic na Colerick

Aina ya 3. FLAGMETIC

- Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
- Ni mabingwa wa kuahirisha mambo
- Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe
- Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao

Ni watu wa aina gani hawa?
- Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea
- Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
- Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili
- Ni watu wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hatawaliwa na mifano na takwimu halisia
- Wanapenda kufuatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu)
- Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili
- Ni watu wasioumizwa kufanya makosa
- Hawapendi kuwaamini wenzao
- Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo mbalimbali

Mengineyo ni;
- Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika
- Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao).
- Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)
- Ni wagumu wa kuomba msamaha (mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi) ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi sana kuamka)
- Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera, vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera walizozipokea.

Sifa zao zaidi;
- Si watu wanaojali muda na ratiba
- Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyote pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.
- Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani
- Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao
- Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao)

Wanafanyaje mambo yao?
- Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani
- Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu)
- Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko
- Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama
- Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers)
- Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote
- Hawapendi kuelekezwa na mara nyingi eidha huwadharau viongozi wao ama hutengeneza mitazamo na hoja za kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao.
- Wanapenda kutekeleza maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuiya
- Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.

Aina ya 4. COLERICK

- Wana uwezo wa kawaida kiakili
- Ni wa wakali na wakaidi
- Hawana huruma wala unyenyekevu
- Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa
- Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote
- Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa
- Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa
- Watu wasiokata tamaa mapema
- Wanajiamini kupita kiasi
- Hawana uoga ni majasiri sana
- Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
- Kundi la watu wenye nguvu nyingi
- Ni madikteta
- Hawapendi kabisa kupingwa wala kukosolewa
- Watu wa kulipiza visasi
- Watu wa vitendo kuliko maneno
- Ni waonevu, wanapenda dhuruma na ubabe
- Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
- Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani eneo fulani
- Wanafaa sana kuwa viongozi kutokana na uhodari wao wa kuwaongoza watu kwa sera za ushawishi wenye mlengo wa kiukandamizaji
- Hawajui kubembeleza
- Hawaongei wala kucheka ovyo
- Wanapotenda jambo huwa wanawaza namna ya kunufaika na hata kama akimsaidia mtu anawaza namna ya kurudishiwa hicho alichokitoa
- Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa kutokana na uimara wao katika kuthubutu kutenda mambo na hali zao za kutoogopa hasara
- Si watu wanaopenda suluhu na amani
- Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
- Hawapendi starehe kwa wingi
- Ni watu wanaoweza kufurahia mazingira yenye dhiki na shida
- Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe hata baada ya kufariki
- Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha

- Mifano ya watu wa kundi hilo: Idd Amin, Hitler, etc

Ni matumaini yangu mpaka sasa utakuwa umeshajijua kuwa wewe upo katika kundi gani kati ya haya makundi 4 ya haiba. Kama hukusoma sehemu ya kwanza ya somo hili unaweza kusoma kwa kubonyeza hii link http://mpekestn.blogspot.com/2017/09/itambue-haiba-yako.html?m=0


0 comments:

Post a Comment

 
Top