Sunday, 24 December 2017

Tukumbuke tulipotoka huku tukijifunza machache


Si vibaya kukumbuka tulipotoka huku tukijifunza machache

Kuna msemo unasema ukikaa na mwizi na wewe utakuwa mwizi, why? Ni kwa sababu atakufundisha tabia hiyo na wewe utajikuta una adapt mazingira yale na wewe unakuwa mwizi ( but siyo lazima uwe mwizi, utakuwa tu pale utakapokubaliana na hali ile )
Hivyo basi kwa mtazamo wangu naona ukikaa na wenye maarifa na wewe utakuwa na maarifa na hii ni pale tu utakapokuwa na juhudi kuiga kufanya kama wale wenye maarifa wanavyofanya, the same ukikaa na tajiri, kama na wewe utaiga na kufanya yale tajiri anayoyafanya hakika na wewe utatajirika na kuwa kama yeye.

Kuna mmoja aliwahi kusema "Kuzaliwa masikini siyo kosa lako ila kufa masikini ni kosa lako tena kubwa."
Haimaanishi ukizaliwa kwenye familia masikini kuwa na wewe utakuja kuwa masikini, the same ukizaliwa kwenye familia tajiri siyo guarantee ya wewe kuja kuwa tajiri. Unaweza ukazaliwa kwenye familia ya mambo safi lakini ukafa masikini vilevile kama usipojitambua.

Zamani tulikuwa tunasikia kuwa mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe ila kwa sasa hivi mtaji wa masikini ni akili yake mwenyewe. Na ndo maana sasa hivi unaweza ukawa nyumbani kwenu ukaingia mtandaoni ukaagiza chakula wakakuletea mpaka mlangoni pako.

Zama zimebadilika ngudu yangu hivyo na wewe unatakiwa ubadilike kwa maana pasipo kubadilika utashangaa hupigi hatua kwenda mbele na kujikuta kila siku uko maala pale pale.

Pia kumbuka Mungu ndo mpaji wa kila mtu, usiache kutengeneza mahusiano yako vizuri na yeye kama unataka kufanikiwa.

No comments:

Post a Comment