Thursday, 30 November 2017
Hatua za kuzivuta fursa
Fursa zipo kila mahala na fursa ni matatizo yaliyopo katika jamii inayotuzunguka. Je ni jinsi gani unaweza ukazivuta hizo fursa!!! nimekuorodheshea njia kuu mbili za kufanya ili fursa zilizopo katika jamii zikufuate, nazo ni..
1. Wekeza kwenye kujenga jina lako.
Jina linalipa kama utaliwekeza vizuri mfano kama ukisikia mtu anamtaja Diamond utajua kuwa ni mwanamuziki, au akitajwa Masanja kila mtu anamjua au Milard Ayo, au Bhakhresa. Hawa wote wanajulikana na hii yote ni kwa sababu waliwekeza kwenye majina yao na ndiyo maana wanajulikana na kila mtu, hivyo kusababisha fursa nyingi kuwafuata kwa sababu ya majina yao kujulikana. Ili jina lako likae vizuri unahitajika ulilishe kwanza ( Ugharamie kwa kutumia hela, muda au nguvu zako ) ili nalo lije likulilishe baadaye. Hao wote niliowataja hapo juu na wengineo wengi ambao sijawataja wamekuwa maarufu kwa sababu wamewekeza kwenye majina yao. Je wewe likitajwa jina lako linajulikana na wengi! Na unajulikana kama nani? Au ni mtu yule ambaye jina lako linajulikana na marafiki zako tuu, au wafanyakazi wenzako au wanafunzi wenzako tuu!!!. Ili kuweza kuzivuta fursa nyingi jina lako linatakiwa lifike hata mahala ambapo wewe haujawahi kufika ( Jina lako linatakiwa likutangulie kabla wewe haujafika ) ili likutengenezee mazingira mazuri ya kuzivuta hizo fursa ( watu wakusikie kabla hawajakuona )
Tengeneza mkakati wa kukuza jina lako na kile kilichobebwa na jina lako.
Kumbuka: Jina lako lina thamani kuliko mali ulizonazo. Ukiwa na jina kubwa litakutengenezea mazingira ya kuaminika na watu na hivyo kuweza kukushirikisha mambo mengi.
2. Kuzingatia ubora katika kazi zako.
-Kazi zako zinatakiwa zionekana ( How visible is your vision? ) na watambue kitu unachokifanya kwa kupitia matangazo. Usikae kimya kwa kusema eti kwa sababu nipo hivi watu watakujua hapana unatakiwa ujitangaze.
Watu waone ubora wa kazi yako, pamoja na matangazo juu ya kazi yako unatakiwa pia uoneshe ubora juu ya kile unachokifanya ndipo fursa zitakapokujia.
Jinsi huduma yako inavyoweza kupatikana ( Accessibility ) Muonekano wa eneo la kazi yako pawe ni mahala pazuri ambapo hata wateja wako watapenda kuja.
Hela haileti maono ila maono yanaleta hela. Nikutakie siku njema
No comments:
Post a Comment