• Maisha ya kipindi hiki ni tofauti na maisha ya miaka iliyopita, zamani walikuwa wanasema mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe ila kwa sasa hivi ukiutumia huo msemo utakuwa masikini kwa sababu sasa hivi ili ufanikiwe unahitaji kutumia akili hivyo kwa sasa hivi tunasema mtaji wa masikini ni akili yake mwenyewe. Kwa hiyo sasa hivi ili ufanikiwe haitaji uwe na nguvu bali unahitaji uwe na akili ya kuwavuta watu kwako kwa maana hao watu ndo mtaji wenyewe.
  • Kwa zamani ukiwa na elimu tu unaweza ukafanikiwa kwa sababu ukimaliza tu kusoma kazi inakusubili unaajiriwa ila kwa sasa hivi, ukiwa na elimu kama hauna akili ya kuitumia hiyo elimu yako hauwezi ukafanikiwa. Hivyo unatakiwa ufikilie zaidi ya kusoma ili uweze kuitumia elimu yako kujiajili.
  • Maisha yamebadilika using'ang'anie tu kujifunza elimu ya darasani bali pia ili ufanikiwe unahitaji uweze kujifunza na elimu dunia ( elimu ya ujasiriamali ) maana hiyo ndiyo inanafasi kubwa sana ya kukutoa kimaisha kuliko hiyo elimu ya darasani. Acha uvivu wa kusoma vitabu, kuna msemo unasema eti ukitaka umfiche utajili muafrika muwekee katika maandishi. Ni kweli waafrika wengi hatupendi kusoma vitabu, na hapa ndipo wenzetu wazungu wanapotupitia kwenye mafanikio maana wenzetu wana tabia ya usomaji wa vitabu tofauti tofauti vinavyohusu mafanikio. Na vitabu hivyo  vimebeba siri kubwa za mafanikio, tangu nimeanza tabia ya kusoma vitabu mpaka leo nimejifunza mambo mengi sana. Nakushauri na wewe anza kusoma vitabu kuanzia leo utaona mabadiliko. Pia kumbuka kutendea kazi vile unavyovisoma.

         Law of success. INFORMATION + APPLICATION = TRANSFORMATION
  • Mwisho: Mungu ndo msimamizi wa kila kitu katika mipango yako yote unayopanga kufanya, hivyo usimsahau yeye kwa maana ndio mtoa baraka kwa kila mtu




2 comments:

 
Top