Ubongo ni kitu cha thamani sana ambacho Mungu amekiumba kwa binadamu, na amempa kama zawadi ili akitumie aweze kufanikiwa katika maisha yake. Lakini ubongo huo huo kama utautumia vibaya unaweza ukakufanya kuwa masikini milele. Ikumbukwe kuwa ubongo wako hauwezi kuwaza jambo ambalo lipo nje ya uwezo wako. Unapowaza wazo la biashara unatakiwa uanze bila kuogopa wala kusubili eti mpaka uwe na pesa ndipo uanze. Anza kidogo kidogo kwa maana hata Mungu amesema kuwa mwenye nacho ataongezewa, Je wewe unacho nini ulichokianzisha mpaka uongezewe?
Kama umepanga kujiendeleza kusoma fanya hivyo, kama umepanga kujiendeleza katika kipaji chako fanya hivyo, wakati ndo huu usisubilie kesho. Na katika kila kitu unachokifanya hakikisha unakifanya kwa bidii na kwa ubora. Tumia ubongo wako kuwaza vitu chanya na siyo hasi. Usiwaze kushindwa,  waza kushinda.
Ni matumaini yangu utaanza kuutumia ubongo wako vizuri. Nikutakie tafakari njema

1 comments:

 
Top