Wanandoa
wawili Bi Ester na mume wake Bw Jonathan waliokuwa wakipendana sana waliishi
miaka mitano ndani ya ndoa yao kwa amani sana, miaka yote hiyo walikuwa
wanapendana sana, japokuwa kukwaruzana ndani ya mahusiano ni jambo la kawaida
lakini walihakikisha wanayamaliza mambo yao kimyakimya ili kutowapa faida watu
wa nje, Miaka ilizidi kukatika, hatimae bi Ester akabeba ujauzito, Bahati mbaya
baada ya ujauzito ule kufikisha miezi minne tu mumewe Jonathan aliugua sana
ugonjwa wa ajabu, kwani alikuwa akianguka ovyo na kuanza kukimbia peke yake,
hakuwa na tofauti na mwehu muda huo, uzuri Jonathan alikuwa na ndugu wengi
ambao baada ya kupata taarifa kuwa ndugu yao ameugua walijazana kwa wingi
nyumbani kwa Jonathan,, Wakati huo wote bi Ester alikuwa akimuuguza mumewe na
kupambambana na misukosuko ya hapa na pale, alikubali hata kumshikilia mumewe
asiweze kukimbia kwani alionekana kichaa kabisa muda huo, hakujali hata kama
alikuwa na mimba ambayo ilikuwa inahitaji matunzo pia ila alipambana
kuhakikisha mumewe Bw Jonathn anapona..
************************
Hadi
ndugu zake na Jonathan wanakusanyika, bi Ester alikuwa ameshaleta daktari
aliyekuwa anamtibu Jonathan palepale nyumbani, kwa kuwa Mungu aliwajaalia uwezo
wa mali swala la kumuuguza mumewe halikuwa gumu sana, hakujali kama mali
zitaisha alichojali muda huo ni kuhakikisha anapambana na mauti yaliyokuwa
mbele ya mumewe labda mungu mwenyewe atamchukue ila siyo kifo kisababishwe na
ukosefu wa mali, Alidiliki hata kugombana na ndugu zake na Jonathan
walipojaribu kumgombeza kuwa anaharibu mali kwa ajili ya matibabu ya mumewe,
haya ni baadhi ya maneno aliyoongea kaka yake na Jonathan akimwambia Ester nanukuu kidogo
"shem,
hizo pesa unazotupa kumtibu mumeo si uziache tu ili zisaidie msibani, mdogo
wangu hawezi kupona na nakuona kabisa unavyozitolea macho mali zake"
Bi
Ester hakujibu kitu zaidi ya kusimama na kwenda kumuinua mumewe aliyekuwa chini
baada ya kuanguka, wakati anampeleka mumewe ndani ghafla alimuona kijana mmoja
ambaye alikuwa amepauka sana, kijana yule alimsalimia Ester na Ester akaitikia
kwa upole, kijana yule bila kujali kama bi Ester alikuwa anahangaika na
mgonjwa, alijikuta akitoa shida yake hapohapo, namnukuu
"Samahani
dada, hapa nilipo nilikuwa na wenzangu tunatoka field lakini tulivamiwa mstuni
tulipokuwa tunafanyia field, tumenyang'anywa kila kitu, na hapa nimetembea
kutoka mstuni hadi hapa kwa mguu, naomba unisaidie hela kidogo ya kunirudisha
nilikotoka au chakula nile, maana sina ndugu yeyote anayenifaa zaidi ya mama tu
ambaye naye ananitegemea mimi kwa kila kitu halafu yupo mbali na hapa, hata
simu hana na hajui kama mwanae nimepata tatizo"
Alizungumza
kijana yule maneno ambayo yalimgusa sana Bi Ester ambaye naye alikuwa amebaki
na mama tu baada ya baba yake kufariki, ubaya zaidi hata mama yake alikuwa
akimtegemea yeye tu licha ya kuwa na watoto wengi ambao hawakuwa na msaada
wowote kwa mama yao.
***********************
Bi
Ester alimuangalia kijana yule kwa huruma kisha akamwambia asubiri, alishangaa
kwanini Mungu anampa majaribu namna ile na kupitia wakati mgumu kama ule,
alimpeleka mumewe na kumlaza ndani huku yeye akiingia chumbani kwake na kuvuta
droo akachukua pesa kiasi na kutoka nje, alipofika alimpa kijana yule ambaye
hakuamini, alimuangalia mara mbilimbili bi Ester,
"Wahi
sasa ukatafute usafiri maana unakoenda ni mbali sana"
Alizungumza
Ester na kumfanya kijana yule kutoa machozi ya furaha kwa kutoamini, alimuaga
Ester huku akimpa maneno mazuri kwa kumuahidi Mungu angetenda muujiza mkubwa
sana kwa mgonjwa wake kisha akaondoka,
Ilipita
wiki moja tu kama utani Hali ya Jonathan ikatengemaa kabisa, ugonjwa uliokuwa
unamsumbua ukapona kabisa na kumfanya Ester na nduguze Jonathan kujawa na Furaha.
BAADA YA MIEZI MIWILI
Ilipita
miezi miwili, ule ugonjwa aliokuwa ameugua Jonathan ukampata Ester,Jonathan
alijikaza kumhudumia ester kwa wiki moja tu ya kwanza, ndugu zake wakaanza
kumwambia anaharibu mali, wapo waliomwambia kuwa Ester ndo alimloga mumewe mara
ya kwanza na sasa ugonjwa umemrudia yeye, Jonathan hakukumbuka tena fadhila
alizotendewa na mkewe alipokuwa mgonjwa, alichoangalia ni mali yake na hakutaka
kuendelea kuiharibu kumuuguzia Ester, alichokifanya ni kumrudisha Ester kwa
mama yake ambaye nae alikuwa hana uwezo na alikuwa akimtegemea sana mwanae
kwenye mambo mengi.
********************
MAma
Ester hakuwa na uwezo wa kumzuia Ester kukimbia kwani tayari alikuwa
ameshazeeka, Ester alikimbia na mimba yake na kuanza kuzulura barabarani kama
mwehu sasa, miezi miwili mingine ilikatika huku Mama ester akimtafuta mwanae
kila kona bila mafanikio, wakati huo Ester akiwa chini ya ghorofa kubwa la
wahindi alikuwa akilia kwa maumivu makali ya tumbo la kujifungua wakati huo
kuna gari ilipaki karibu na yeye, alishuka kijana mmoja akiwa na bahasha ya
khaki mkononi, alipomuona Ester alijikuta akiangusha bahasha ile huku
akikimbilia haraka ndani ya ghorofa lile, na baada ya muda alirudi akiwa na
vijana wenzake wasiopungua watatu,walimbeba Ester na kumuingiza ndani ya gari
huku kijana yule akiondoa gari kwa kasi sana.
huku
nyumbani kwa Jonathan baada ya kumfukuza Ester alioa mwanamke mwingine ambaye
alikutana naye kwenye mihangaiko ya biashara,,,laiti angejua mwanamke yule
hakuwa mtu wa kawaida asingethubutu, kama kawaida ya mapenzi mapya baada ya
kumuoa tu alimueleza siri zake nyingi sana.
BAADA YA MWEZI MMOJA
Mwezi
ulikatika wakati huo Ester ndo akili za kawaida kumrudia,alishangaa kujikuta
akiwa amelala kwenye kitanda cha hospitalini,alipoangakia pembeni alimuona mama
yake mzazi akiwa amebeba katoto kadogo,,
"Mamaaa
nimefikaje hapa"?
aliuliza
Ester ila kabla hajajibiwa kuna kijana aliingia akiwa amevaa nguo za kidokta,
alimsalimia Ester na kumpa pole wakati huo Ester akiwa anashangaa,kija
na
yule alianza kwa kujitambulisha
"Bila
shaka umeshanisahau,Mimi ndo yule kijana ulinisaidiaga pesa kipindi fulani
nilipokuja kwako nikiwa natoka field baada ya kutekwa na majambazi mstuni"
baada
ya maneno yale Ester alikumbuka kila kitu na kujikuta akibubujikwa na
machozi,kijana yule alijitaidi kumbembeleza Ester hadi akanyamaza,,
"Nitaishije
na mtoto wangu jamani,mama yangu pia ananitegemea Mimi,mume wangu kanifukuza
kisa kuugua kwangu,,,eeeh Mungu weeee"
alilia
Ester
Usilie
Dada, kwakuwa hauna kazi nitasubiri mwanao akue kidogo nitakufungulia mradi,pia
kuhusu sehemu ya kuishi usijali,kuna nyumba nimenunua ina vyumba vingi utakuja
kuishi pale na mama"
alijibu
kijana yule
Ester
alimungalia sana kijana yule kwa kutoamini ila alishangaa kumuona mama yake
akiinuka akamsogelea mwanae akamshika mkono na kumwambia,,,
"Ni
kijana mzuri sana, ndiye aliyelipia pia gharama zote za matibabu na
amenihudumia wakati wote ulipokuwa mgonjwa"
hapo
ndipo Ester akakumbuka alikuwa mgonjwa kweli,alisimana akamkumbatia yule kijana
huku kila mmoja akitokwa na machozi
BAADA YA MIEZI MITATU
Baada
ya miezi mitatu tayari Ester alikuwa kwenye duka kubwa la nguo alilofunguliwa
na kijana yule huku akiishi kwenye nyumba nzuri ya kijana yule na mama yake na
mtoto wake.
Siku
moja akiwa dukani kwake, alishangaa kumuona yule kijana akipaki gari yake huku
akimwambia Ester funga duka maana kuna tatizo imetokea,Ester alifunga haraka
wakaingia ndani ya gari na kuondoka, baada ya muda walifika hospital kijana yule
alimvuta mkono na kuingia kwenye moja ya chumba cha wagonjwa mahututi, moyo
ulimuenda mbio Ester baada ya kumuona mumewe akiwa amelazwa,Jonathan alipomuona
mkewe alimuangalia kwa jicho regevu kwani hakuwa na nguvu tena kutokana na
majeraha makubwa aliyokuwa nayo mwili mzima yakionekana ni majeraha ya moto,,
"nisamehe
mke wangu, nilikuacha kwa kudhani utamaliza mali zangu kwa ajili ya kukutibu
kumbe nilikuwa najidanganya maana baada ya kukuacha nilioa mwanamke mwingine
ndo aliyenifanyia hii njama na kuiba mali zote kisha akachoma moto nyumba ili
kuondoa ushahidi, ila nashukuru wamemkamata wakati anataka kukimbia"
alizungumza
Jonathan kwa shida huku akishika mkono wa mwanae, wakati anaushika tu, hapohapo
akanyamaza kimya na kupoteza maisha.
Ester
aliangua kilio kwani alikuwa bado anampenda sana mume wake, alimgeuk
ia
kijana yule akamkuta naye akilia kwa uchungu
"pole
dada nilipomuona nimemtambua kuwa ni mumeo kwani ndo nilikuta unamhudumia
kipindi kile, nashangaa ulipougua wewe alishindwa kukumbuka fadhira zako, hili
nimejifunza hata Mimi nikioa natakiwa kumuheshimu sana mke wangu kwenye shida
na raha.
alizungumza
kijana yule,,,
FUNZO:
=>Pesa
ni kama maua huwezi kulinganisha na uhai wa mtu
=>Usimtenge
mwenzio wakati wa matatizo kwani hujui kesho yako.
=>Siku
zote wema hauozi, Tenda Wema Leo kwa maana hujui atakae kusaidia kesho.
____SHARE
NA WENZAKO_____
0 comments:
Post a Comment