Katika maisha usimdharau mtu yeyote kwa maana huwezi jua kesho atakuwa nani, na pia ni vizuri kuchagua marafiki wa kuambatana nao ila si vizuri kuwatenga maadui. Wapende maadui zako kwa maana wao ni chachu ya mafanikio yako.
Na pia kumbuka kila mtu uliyekutana naye ana nafasi katika maisha yako na Mungu hajaruhusu mkutane kwa bahati mbaya, haijalishi ni mzuri au mbaya kwako. Yule masikini unayemdharau leo ndo atakuja kununua bidhaa zako utakapoanza kuziuza, na kama unabisha hili, tengeneza bidhaa zako na uzipeleke sokoni au dukani, halafu kusiwe na watu_unadhani nini kitatokea???? Unaweza ukanunua mwenyewe bidhaa zako !!!!. Kama jibu ni hapana, basi haina haja ya kuwadharau wasio nacho
Mwisho napenda kumaliza kwa kusema: kuna watu wamebeba mafanikio yako na huwezi kuwajua kwa kuwatazama, unachotakiwa ni kuishi vizuri na kila mtu ili mwisho wa siku uweze kupata mafanikio yako*

0 comments:

Post a Comment

 
Top