Inaumiza sana..... Baada ya mahusiano ya zaidi ya miaka mitatu na
siku kadhaa kijana alishindwa kuhimili shinikizo la
ndugu na kumwacha mpenzi wake kwa madai
kuwa sio wa hadhi yake. Akapewa mke mpya na
baadae kuanza maisha mapya na ndugu
wakifurahia uamuzi wao wa kumpa kijana wao
mke mpya huku wakimsahau yule dada wa
kwanza.
Binti yule wa kwanza akaondoka na kwenda mji
mwingine kuanza maisha yake huku akijikita
katika biashara zake.
Siku zikapita na kila mtu akasahau mkasa ule wa
binti aliyefukuzwa kabla ya kijana kuanza
kuumwa.
Wakazunguka kila hospitali bila kupata tiba
mpaka pale walipokuja kugundua kuwa figo zake
zimeharibika na hawezi tena kupona kama sio
kupata figo kutoka kwa mtu wa karibu au afe.
Ndugu na marafiki wakamkwepa na kumwacha
akiwa kalala pale hospitalini bila ya msaada na kila
mmoja akiogopa kutoa figo kumpa kijana apone
na mbaya zaidi hata mke wake mpya akawa
amemkimbia na kurudi kwao.
Mama wa kijana alizidi kumtunza kijana akiwa
hana namna ya kumsaidia kwani kwa uzee ule
alikataliwa kutoa figo yake ili amsaidie mwanae
apone.
Siku zikasogea na yule mchumba wa kwanza
aliyefukuzwa akapata habari za mpenzi wake wa
mwanzo kuwa anaumwa na hali yake sio nzuri. Kwa huruma akaenda
mpaka hospitalini na kukubali afanyiwe upasuji na
atolewe figo moja.
Kabla ya upasuaji aliomba karatasi na kuandika
kitu na kumpa daktari amwekee. Kwa bahati
mbaya baada ya upasuaji yule dada alifariki na
kijana baada ya wiki kadhaa alipona na kuwa
mzima kabisa.
Siku moja akaenda hospitali ili amshukuru daktari
na wote waliomsaidia akiwa pale hospitali, akiwa
chumbani kwa daktari alipokea karatasi kutoka
kwa dakatari na kuambiwa kuna mtu aliyemsaidia
kutoa figo kabla hajafa alimwachia karatasi...
Kaka kabla ya kusoma akaumia sana na kusema
laiti mtu huyo angekuwa mzima amshukuru kwa
moyo ule wa huruma na kisha akaifungua ile
karatasi na iliandikwa:-
"Mpenzi wangu Nolesy kama unausoma ujumbe
huu basi ujue wewe ni mzima na umepona sasa
baada ya mimi kukupa figo yangu.
Nilikupa moyo wangu ukauumiza sana na kunipa
majeraha makali huku ukinitazama bila huruma.
Sasa nimekupa figo yangu, naomba uipende sana
hata kama hautaniona mimi kama ilivyokuwa kwa
moyo wangu.
Nakutakia maisha mema.
Zilipendwa wako Habiba"
Siku moja baada ya kuusoma ule ujumbe kijana
yule siku ya tatu yake alikutwa amekufa kwa
kujinyonga.
Rafiki shikilia ulichonacho sasa kwa maana ni
baraka kwako na huwezi ona umuhimu wake
mpaka utakapokipoteza au kukikosa kabisa

0 comments:

Post a Comment

 
Top