Aliingia ndani ya nyumba na kukuta mkewe akiwa na huzuni, hasira iliyochanganyikana na jazba.
"Hey babe" alimuita huku akiweka gazeti lake katika meza iliyokuwepo pale sebuleni. " Sema" mke alimjibu kimkato huku akivua viatu vyake.
"Na wewe ndio umeingia mida hii?" Mume alimuuliza mkewe huku mkewe akielekea lilipo jokofu kuchukua maji ya kunywa.
"Ndio" mke alijibu.
"Watoto je?" Mume aliuliza tena.
"Wako chumbani kwao kuoga na kubadili nguo" mke alimjibu huku akichukua vile viatu vyake na kuweka sehemu ya kutunzia viatu karibu na mlango.
"Uko sawa?" Mume alimuuliza.
"Ndio" mke alijibu.
" Hapana hauko sawa. Unaonekana kabisa hauko sawa babe. Tafadhali ongea na mimi tatizo ni nini mpenzi" mume alimwambia huku akimsogelea mkewe karibu zaidi.
"Aah! Wewe nawe na maswali yako mengi mimi nimeshayachoka. Hauwezi kuniacha hivi bwana? Leo nimekua na siku mbaya sana siko sawa wewe niache tu!" Mke alimjibu mumewe.
Mume akamtazama mkewe akielekea jikoni. Akaanza kusikia sauti za vyombo vikioshwa ktk sink na kuwasha moto ili aanze kupika. Unataka kuanza kupika? Mume akauliza huku nae akimfuata mkewe jikoni.
"Wewe unaona ninafanya nini? Maswali yako mengine ni ya kitoto kweli Baba James. inatosha sasa" mkewe alimueleza.
"Usianze kupika saa hizi. Njoo. Twende chumbani" mume alimwambia mkewe huku akimshika mkono waondoke.
"Muda umeenda sana. Natakiwa nipike haraka vinginevyo watoto watachelewa kula na hvyo kuchelewa kulala. Sina muda" mke alimgomea mumewe.
"Please wife, wewe twende. Mimi nitakusaidia" mume aliongea.
" Kama ni tendo la ndoa, siko katika mood kabisa." Mke aliongea huku akichukua mchele uliokuwemo kwenye kabati.
"Mpenzi wangu please" mume aliongea huku akimshika mkono mkewe. Mkewe alimpa mkono na mume akazungusha mkono kiunoni kwa mkewe na kuanza kuelekea chumbani kwao.
Wakaingia chumbani. Mume akafunga mlango.
"Unaweza kuungana na mimi kumuabudu Mungu kidogo? tafadhali naomba tupige magoti tumuombe Mungu kwa dakika chache mpenzi wangu" Mume alimwambia mkewe huku akiwa ameegemea mlango.
Wote wakapiga magoti na wakaanza kumuabudu Mungu. Mume akaanza kuimba na mkewe nae akajiunga nae. Wakaanza kusali kwa pamoja. Mke akaanza kuinua mikono juu huku akiomba na kuongea na Mungu wake.
Mume akamnong'oneza mkewe na kumwambia "ni muda wako huu sasa wa kuongea na Mungu kuhusu ya kuudhi yaliyokutokea leo, yeye ni muaminifu atakurudishia tena furaha yako"
Midomo ikawa ikicheza. Sauti haitoki. Macho yakiwa yamefumbwa. Machozi yakitelemka mashavunu mwake. Tabasamu likiwa kwa mbali. mke akainua mikono juu na kuanza kuomba;
"Asante baba yangu wa mbinguni kwa neema na rehema. Kwa kubeba mizigo yangu yote, kwa kuwa mwamba wangu usiotikisika. Asante kwa kunipa mume bora anaenikumbusha kukuabudi na kukusifu wewe pale ninapokua na furaha hata ninapokuwa nimelemewa na maudhi ya binadamu.
"Mume ambae ananirudisha kwenye mstari pale ninapokuwa busy na haya ya kupita ya duniani hapa kazi na biashara ambayo si kitu bila ya wewe. Ndio maana ninalitukuza jina lako kwani ninavyokuabudu wewe unanirudishia furaha yangu.
"Nisamehe Mungu wangu kwa kumuonyesha hasira mume wangu, kila alichokuwa akikifanya leo ni kuonyesha jinsi gani ananijali mkewe. Sikutakiwa kumjibu kwa hasira kwani sio yeye alionikosea. Juu ya jina lako lipitalo majina yote ninaomba nikiamini AMEN!!
Mume akainuka na kumbusu mkewe kwenye paji la uso na kumwambja haya;
"Saa hizi unaonekana ukiwa poa. Nimekusamehe mke wangu. Maisha yana mabonde na milima. Unaweza ukajikuta hutaki kuongea na mtu kabisa kwa sababu ya kuudhiwa, lakini tafadhali sana ongea na Mungu. Acha mambo mnengine yote yasubiri, ongea na Mungu. Usiwe busy sana mpaka umsahau Mungu, kwani kwa kufanya hivyo unamkaribisha shetani kuja kukuharibu.
Mke akajisogeza kwa mumewe na kumbusu mdomoni kimahaba zaidi. Akamkumbatia na kujilaza kifuani kwa mumewe. Mumewe akaanza kumchezea nywele zake huku mke akimsimulia jinsi gani alivyokua na siku ngumu, hasara hasara aliyoipata baada ya mali aliyonunua kuharibika, kuibwa kwa 'power window' ya gari yake na purukushani zingine za siku nzima.
Mke akajisikia akiwa salama mikonon mwa mumewe. Akacheka..akatabasamu.
"Ok honey, twende tukapike. Nitakusaidia kupika. Wewe utapika wali mimi nitapika mboga" mume akaongea.
Wakainuka na kuelekea jikoni, wakaanza kupika huku wakiimba na kutaniana. Watoto wakawa wakiwatazama wazazi wao wakicheka na kuimba kwa pamoja.
Chakula kikawa tayari haraka na ilikua ni furaha kukitengeneza kwa pamoja, wakaungana na watoto wao kwenye meza. Wakala kwa furaha kama familia.
Wakaenda kuwalaza watoto wao, na wao wakaelekea kulala. Usiku ule Wakapeana chakula cha wanandoa kwa furaha na amani tele.
Mungu abariki ndoa yako, Mungu abariki mahusiano yako yakawe yenye kuleta tija, ukajenge familia yenye amani, mshikamano na upendo.
Mke akajisikia akiwa salama mikonon mwa mumewe. Akacheka..akatabasamu.
"Ok honey, twende tukapike. Nitakusaidia kupika. Wewe utapika wali mimi nitapika mboga" mume akaongea.
Wakainuka na kuelekea jikoni, wakaanza kupika huku wakiimba na kutaniana. Watoto wakawa wakiwatazama wazazi wao wakicheka na kuimba kwa pamoja.
Chakula kikawa tayari haraka na ilikua ni furaha kukitengeneza kwa pamoja, wakaungana na watoto wao kwenye meza. Wakala kwa furaha kama familia.
Wakaenda kuwalaza watoto wao, na wao wakaelekea kulala. Usiku ule Wakapeana chakula cha wanandoa kwa furaha na amani tele.
Mungu abariki ndoa yako, Mungu abariki mahusiano yako yakawe yenye kuleta tija, ukajenge familia yenye amani, mshikamano na upendo.
0 comments:
Post a Comment