Siku zote tumekuwa tukilaumu kuwa maisha ni magumu, nikukumbushe kuwa wewe ni sababu ya mawazo yako na juhudi yako pia, na yule unayemuona amefanikiwa na ni tajiri leo ni sababu ya mawazo yake na juhudi zake pia. Kwa nini unafikilia kuwa maisha mazuri wameumbiwa baadhi ya watu na siyo wewe!!! Hebu fikilia unautumiaje muda wako katika kufanya shughuli za kimaendeleo, au unashinda kwenye mitandao ya kijamii siku nzima halafu ikifika usiku unalaumu maisha magumu.
Wewe ni msomi, sawa sikatai, ila unatumiaje elimu uliyokuwa nayo katika kujiendeleza? Au ndo unajua kusolve dy na dx tu na kusubili kuajiliwa kwenda ofisini. Unaujaza nini ubongo wako? Inspiration au maneno ya kukatisha tamaa! Maana wengine wao hata wakiangalia move wanaangalia move za kutisha tu. Kwa nini usiwe unaangalia move zitakazo kushawishi katika mafanikio na pia ukasoma vitabu ili uongeze maarifa.
Kumbuka miaka inaenda na umri unazidi kusogea na uzee unakuita, cheza na alama za nyakati. Kile kitu unachokiona kuwa kinaweza kukuingizia kipato anza kukifanya leo usisubili kesho.
Badilika sasa
0 comments:
Post a Comment