Nimejisikia kuongea kitu hiki leo: Je ushawahi kujiuliza ni kwa nini upo hapo ulipo!!! Au ni vitu gani vinakusababisha uwepo hapo ulipo!!! Binadamu wengi tupo hivi leo ila hatutaki kujiuliza ni kwa nini Mungu ametuacha tuwe hai, au je wote waliokufa ni kwamba walimaliza majukumu yao hapa duniani. Lahasha! Wengi wamekufa na ndoto zao na hii ni kutokana na ule msemo wa kusema muda bado upo, nitafanya kesho. Fanya leo maana hamna aijuae kesho.
Kila mtu ana nafasi yake hapa duniani: Amka, jitambue na ubadilike, anza kutimiza ndoto zako leo maana muda huusubili. Hukuletwa Duniani kuja kupunga upepo au kushangaa majengo! Bali umeletwa ili uje kuwa mtu fulani na katika nafasi hiyo uweze kumtumikia Mungu.
Angalia aina ya marafiki uliokuwa nao, jiulize je ni marafiki faida au marafiki hasara, kumbuka siyo kila rafiki yupo kukujenga wengine wapo kwa ajili ya kukuharibia future yako. Kuwa makini sana na watu unaochagua kuwa nao mara kwa mara. (Kampani yako).
Na pia nimalizie hili kuwa, ukifuata hayo yote, jambo lililo muhimu zaidi ni KUMTEGEMEA MUNGU maana yeye anajua ni wapi wewe unatakiwa kuwepo na ni kwa muda gani. Mtegemee uku ukifanya yanayompendeza yeye.
Uwe na tafakari njema
Uwe na tafakari njema
0 comments:
Post a Comment